Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Issue Date
Now showing 1 - 20 of 53
Results Per Page
Sort Options
- ItemStatus of Mercury Concentration in Mudskipper Goby (Periophthalmussobrinus) Found in Zanzibar Intertidal Areas(THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR, 2010-12) Hamad, Zainab AliMarine pollution by heavy metals is a worldwide issue of concern today. Improper waste disposal in Zanzibar, especially electronic waste that releases different chemicals such as Arsenic, Chromium, lead and mercury to the environment, together with agricultural activities, tanning and municipal waste which contain harmful chemicals poses a threat to aquatic environment. The present study aimed to determine the concentration of total mercury concentration in goby fish (Periophthalmussobrinus) tissues found in Zanzibar Islands. A total of 75 fish were collected during low tides at four sites found in Unguja Island which are Bumbwini, Kilimani, Kinazini and Malindi. Twenty fish were captured per site, except Kilimani intertidal area where only fifteen fish were collected due to weather conditions. The collected fish were first stored at – 20 0C refrigerator and then dissected and lyophilised (freeze-dried) by using Labconco Freezone 2.5 L freeze drier for sampling analysis. The total mercury concentration of fish tissues was analysed by using DMA-80 Direct Mercury Analyser with the DORM 4 certified reference material. Data showed that the total mercury concentration in fish samples did not exceed the standard set by of 0.5 mg/kg dry weight of methylmercury concentration. However, three goby fish collected at Bumbwini intertidal area were found to have total mercury concentration which range from to 0.224 -0.2811(mg/kg) which exceed the 0.2 mg/kg allowable limit of total mercury concentration for vulnerable groups (frequent fish consumers, pregnant women, and children under 15 years old).The correlation between total mercury concentration with fish weight and length was evaluated by using Pearson correlation model. Comparisons yielding probability values of less than 0.01 were considered to demonstrate the correlation. Overall, there was a positive correlation between fish length and total mercury concentration but not significant; except for the fish collected at Kilimani intertidal area, which showed significant positive correlation between fish length and total mercury concentration (correlation= 0.932, p =0.000). However, the fish collected at Malindi intertidal area shows negative significant correlation between fish length and total mercury concentration(correlation = - 0.653, p =0.002).Generally these results suggest that the goby fish from Bumbwini, Kilimani, Kinazini and Malindi are safe for human consumption but this is an alarm of mercury contamination to the coastal marine ecosystem of Zanzibar.
- ItemMuundo wa Lugha Katika Maishairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar(The State University of Zanzibar, 2017-11) HAMAD, Asha MheneUtafiti huu unahusu “Muundo wa Lugha katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar”. Diwani nne za watungaji wawili wa Zanzibar zilichambuliwa. Diwani hizo ni Kina cha Maisha ya Mohamed (1984) na Jicho la Ndani ya Mohamed (2002). Diwani nyengine ni Andamo iliyoandikwa na Ghassani (2016a) na Siwachi Kusema pia ya Ghassani (2016b). Utafiti huu ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi A, Magharibi B na Wilaya ya Kusini, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zilipatikana kwa njia ya maktaba, usaili kwa wahakiki wa fasihi na hojaji kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Zanzibar. Njia ya maktaba iliwezesha kupata data nyingi za msingi zilizotimiza malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuchunguza vijenzi vya lugha katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki, vilivyoyajenga mashairi ya watungaji wateule wa Zanzibar kimaana na kiujumi. Aidha, utafiti ulichunguza ukiushi wa kanuni za kisarufi katika mashairi hayo na jinsi vijenzi vya lugha vilivyopambanua mtindo. Nadharia ya Umuundo na Umuundoleo zilitumika katika uchambuzi wa data. Utafiti umeonesha kuwa watunzi wote wamevitumia vijenzi vya lugha katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki kuyajenga mashairi yao. Watunzi wote wamevitumia vijenzi vya lugha kwa kuzingatia kanuni za lugha kwa usahihi kulingana na muktadha, mazingira na wakati. Aidha, wamevisarifu vijengo vya lugha kuimarisha sanaa zao kiujumi na kimaana kwa kuzingatia sifa za lugha ya kishairi inayoendana na mkwepo wa sarufi. Hali hiyo imedhihirisha kuwa upo ufungamanifu kati ya vijenzi vya kimuundo na ushairi, kwa kuwa vijenzi hivyo ndivyo vilivyotumika kuyajenga mashairi ya watungaji wateule wa Zanzibar.
- ItemKiwango cha ukubalifu wa Istilahi za Kiswahili za Technolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar :(The State University of Zanzibar (SUZA), 2017-11) IBRAHIM, Ulfat AbdulazizUtafiti huu unahusu “Kiwango cha ukubalifu wa istilahi za kiswahili za Teknolojia ya habari na mawasiliano, Zanzibar: mfano kutoka istilahi za Kilinux”. Utafiti huu umejikita katika kuchunguza mambo matatu ambayo: Mosi, kuelezea ukubalifu wa istilahi za TEHAMA zilizoundwa chini ya mradi wa Kilinux miongoni mwa Wazanzibari. Pili kufafanua matumizi halisi ya istilahi za Kiswahili za TEHAMA kwa watumiaji walioko katika sekta ya elimu Zanzibari. Tatu kubainisha endapo kuna istilahi nyingine za TEHAMA zinazotumika zisizo za Kilinux. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi (NIK) iliyoasisiwa na K.B. Kiingi (1989). Nadharia hii ina sifa maalum ambazo zinasisitiza usasa wa istilahi za lugha, Pia imeweza kujaliza Nadharia ya Istilahi ya Jumla (NIJ) ya Wuester (1931). Ambayo imeeleza kwamba katika uundaji wa istilahi ni lazima muundaji azingatie vigezo fulani vya istilahi zinazofaa, hivyo basi ni Nadharia inayowaongoza wanaistilahi kuunda, kukubali na kukataa istilahi fulani za Kiswahili, hasa zile zisizokuwa na usayansi yaani zile zisizoelezeka kimantiki kwa mujibu wa vigezo tisa vya kisayansi ambavyo hujulikana kama PEGITOSCA ambapo kwa Kiswahili vimefupisha na kuitwa SIZAMASTALIHA yaani usahihi, uiktisadi, uzalishi, umataifa, uangavu, ustaara, utaratibu, ulinganifu na uhalisia. Utafiti huu umefanyika katika taasisi za elimu ya juu zilizoko Zanzibar, vikiwemo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha SUMAIT na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) . Matokeo ya Utafiti yanaonesha kwamba katika maeneo matatu ya kitaaluma yaliyofanyiwa utafiti kiwango cha ukubalifu wa istilahi za TEHAMA za Kiswahili ni kidogo. Sababu kuu ni ugumu na kutoeleweka kimantiki kwa istilahi hizo. Vilevile baadhi ya mbinu za uundaji istilahi zilizotumika zimepelekea kuundwa istilahi ambazo sio rahisi kueleweka. Vilevile mazoea yalioko kwa watumiaji wa TEHAMA ya kutumia lugha chanzi (Kiingereza) pia ni miongoni mwa sababu ya kutokutumika kwa istilahi hizo za Kiswahihili. Aidha kasumba juu ya lugha ya Kiswahili nazo pia ni kikwazo.Kwa mujibu wa utafiti huu istilahi ambazo zimeonekana kukubalika ni zile zilizotafsiriwa au kutoholewa. Pia kuna istilahi ambazo zimezoeleka kutumika zinazotofautiana na zile zilioundwa na mradi (Kilinux). Kwa matokeo haya imebainika kwamba katika jamiilugha ya waswahili walioko Zanzibar hususani wanataaluma, ambao ni watumiaji wakubwa TEHAMA, ni wachache ambao wanakubaliana na istilahi za TEHAMA za Kiswahili zilizoundwa na mradi wa Kilinux. Taarifa hii imeenda sambamba na tathmini nyingine kama vile (Alloni-Feinberg, 1974; Ohly,1979; Mdee, 1980; Mwansoko, 1990; 1993; Sewangi, 1996; Were-Mwaro,2001) zimedhihirisha kuwa baadhi ya Istilahi zilizoundwa rasmi huweza kukataliwa au kutokukubalika na watumiaji wa lugha husika. Licha ya juhudi kubwa ambazo wataalamu wamefanya katika kuisaidia jamii kutumia maarifa haya mapya (TEHAMA) kwa kutumia lugha yao ya Kiswahili, juhudi hizo kwa upande wa Zanzibar zimeonekana kutofanikiwa kama ilivyokusudiwa. Kwa hivyo zoezi la uundaji istilahi lihusishe wanaistilahi na watumiaji wake. Hoja hii imekaziwa nguvu na Mwansoko (1990) kwa kusema, wenye kuhitaji istilahi (watumiaji wa lugha) hawasubiri kuundiwa istilahi na vyombo vya ukuzaji istilahi bali hujiundia istilahi zao wenyewe pale haja inapozuka. Kutokana na hayo, waundaji istilahi wanapaswa kufanya utafiti zaidi juu ya baadhi ya istilahi nyingine ambazo hazijafanyiwa utafiti, ili waweze kuwasaidia watumiaji wa mtandao kwa lugha ya Kiswahili kwa kuunda istilahi rahisi ambazo zitakuwa ni rahisi kueleweka, kukubalika na kutumika vizuri.
- ItemDhamira Zijengwazo na Taswira katika Methali za Wapemba(The State University of Zanzibar (SUZA), 2017-12) KHATIB, Time OmarUtafiti huu umechunguza dhamira zijengwazo na taswira katika methali za Kiswahili. Chimbuko la tatizo la utafiti huu lilikuwa ni kutoshughulikiwa na watafiti suala la taswira katika ujenzi wa dhamira katika methali za Wapemba. Kwa hivyo, utafiti huu umeweza kubainisha matumizi hayo kwa kuonesha taswira mbalimbali ambazo zimesaidia kujenga dhamira kwa jamii ya Wapemba. Mtafiti amekuwa na lengo kuu moja na malengo mahsusi matatu ambayo yote yamemsaidia kugundua taswira mbalimbali zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kuzijenga dhamira za methali hizo. Mtafiti alitumia data za uwandani na aliweza kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni pamoja na wazee, wanafunzi na walimu wa somo la Fasihi ya Kiswahili wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Wete Pemba. Utafiti huu ulitumia machapisho tofauti yakiwemo vitabu na majarida. Data za msingi kwa kuhojiana na watafitiwa ana kwa ana na data fuatizi zimepatikana kutoka maktabani na kwenye mtandao. Nadharia za Uamilifu na Umuundo umetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa methali zimejengwa vizuri na taswira ambazo zimeibua dhamira zilizokamilika. Methali ambazo zimechunguzwa ni pamoja na zile ambazo zimegawiwa kitaswira kimakundi kwa mujibu wa Khatib (2014), kama ifuatavyo: Kizuolojia, kibotania, kijiolojia, kiastronomia, kiteolojia na taswira za vitu vya kawaida. Aidha, matokeo hayo ya uafiti pia yamebainisha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya taswira zijengazo dhamira katika maisha ya jamii ya Wapemba. Kwa vile methali ndiyo hazina kuu ambayo jamii inaitumia hasa wazee kwa kutoa maadili ya jamii, bado jamii ina nafasi yake kuzitumia methali katika maisha yao ambayo ni njia muhimu ya kuwafundishia watoto ambao ndiyo taifa la kesho. Hivyo methali zinahitajiwa zitumiwe kwa kuangalia mjengeko wake wa maneno ambayo ndiyo hubeba taswira zenye lengo maalumu
- ItemMatumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari zake kwa Watoto Zanzibar(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) HAFIDH, Zainab AliUtafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto. Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahili
- ItemSanaa na Mshikamano wa Maudhui katika Vitendawili(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) MOH’D, Moh'd SalimUtafiti huu umechunguza mshikamano uliopo katika sanaa ya vitendawili na maudhui ya vitendawili hivyo. Utafiti umeangalia vipengele vya kisanaa kadhaa kama vile; sauti, mapigo ya kimuziki yatokanayo na urari wa vina na mizani, lugha ya picha na ishara, tamathali za semi na kadhalika. Pia umechambua maandiko mengi yaliyohusu uchambuzi wa kimaudhui wa vitendawili mbalimbali vya ndani na nje ya jamii hii. Uchambuzi huo umesaidia kuviainisha vipengele tafauti vya kimaudhui vinavyojitokeza katika utanzu huu. Dhamira kadhaa zinazosadifu jamii ya Zanzibar zilionekana ingawa ni kwa ufupi mno. Kutokana na uchambuzi wa kifani na kimaudhui uliojadiliwa, mtafiti amepata nafasi ya kuchambua mshikamano unaojitokeza kupitia sanaaa ya vitendawili na maudhui ya vitendawili hivyo. Huku akiegemea misingi ya nadharia ya kijamii na ile ya kimuundo katika uchambuzi wake. Data zimepatikana kwa njia ya mahojiano na majadiliano ya vikundi lengwa na kuchambuliwa kwa njia yya maelezo kutoka katika makundi yote ya watafitiwa. Mshikamano huo umebainishwa kupitia vipengele anuai kama vile; mwelekeo wa kihistoria, kidini, kisiasa, kiuchumi, kimila na kadhalika. Umuhimu uliopo kwenye utafiti huu ni kwamba, katika utaratibu mzima wa kuvifahamu vitendawili panahitajika watu waangaze zaidi mshikamano wa sanaa na maudhui. Kwani sanaa ya vitendawili haikuwekwa kama mitindo tu ya lugha, bali imetomewa ndani yake maudhui maalumu. Hivyo jamii imeshauriwa kutoviangalia vipengele vya kifani na kimaudhui katika upekee wake, bali vichunguzwe katika mshikamano wake. Ndipo ladha ya vitendawili hivyo itakapopatikana. Maana ya wazi ambayo hujikita zaidi katika kutambulisha utamaduni wa vitu. Na maana fiche (ya ndani) ambayo hii hutambulisha utamaduni wa kifikra wa wanajamii husika. Pia kupitia hilo, kutajenga mtazamo mpya wa kuona thamani ya vitendawili kama taaluma maalumu, badala ya kuonekanwa kama mchezo wa watoto au chemsha bongo tu.
- ItemUhalisia wa Utabaka katika Tamthilia ya Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) HAJI, Moh'd IdrisTamthiliya za Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga zimepata umaarufu na kuwa tamthiliya nzuri na imara za mtunzi Khamis. Utafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza uhalisia wa utabaka katika tamthiliya mbili (Janga la Warevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga). Malengo mahsusi ya ufafiti huu yalikuwa ni, kuchambua uhalisia wa utabaka katika kazi za Khamis, na Kuonesha athari inayoipata jamii kutokana na utabaka unaozungumzwa na Khamis. Ili kufanikisha utafiti huu Nadharia mbili zilitumika, Nadharia ya Umaks na Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa. Nadharia ya Umaks ilisaidia kufafanua aina za utabaka katika kazi za tamthiliya za Khamis, na nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa nayo ilitumika kuchambua athari za utabaka katika jamii. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni maktaba. Data zilizokusanywa zimechambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha hali halisi ya Utabaka katika jamii. Mtokeo ya utafiti yanaonesha kwamba utabaka unaojitokeza zaidi katika tamthiliya za Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga ni utabaka wa kiuchumi, kisiasa, kiitikadi na utabaka wa hali na hadhi. Athari zilizobainika ni kuibuka kwa migogoro katika jamii, umasikini, ufisadi, ukiukwaji wa haki katika jamii na utafutaji wa haki kwa nguvu ya umma.
- ItemUdondoshaji katika Lahaja za Kipemba(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) ABDALLA, Maryam MsabahUtafiti huu umelenga kuchunguza udondoshaji katika lahaja za Pemba. Lengo hili limefikiwa kwa kupitia malengo mahususi ambayo ni kubainisha aina za udondoshaji katika lahaja za Pemba, kufafanua mazingira ya utokeaji wa udondoshaji katika lahaja za Pemba na kubainisha kategoria za maneno ambazo hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Nadharia zilizotumika kuongoza utafiti huu ni nadharia ya Umuundo na nadharia Jumuishi. Kwa upande wa nadharia ya Umuundo, msingi wake mkuu ni kuwa mfumo lugha ni mfumo changamano ambapo ndani yake kuna mifumo mengine tafauti yenye kuhusiana inayoanzia katika kiwango cha sauti, mofimu, neno, virai, vishazi, sentensi, hadi kufikia mshikamano wa sentensi na maana. Msingi mkuu wa nadharia Jumuishi ni kuwa jamiilugha inajengwa na wale watu wanaojiona na kutambua wenyewe kuwa wao wanatokana na jamiilugha moja, ambayo iko tafauti na jamiilugha nyengine. Data za utafiti huu zimepatikana kwa njia ya kusoma maandiko, usaili, uchunguzi makini, uchunguzi shirikishi na usimulizi. Utafiti huu umebaini kwamba kuna aina nne za udondoshaji katika lahaja za Pemba. Aidha udondoshaji katika lahaja za Pemba hutokea katika mazingira tafauti. Data zimeonesha kuwa aina saba za maneno hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Mtafiti amependekeza tafiti zaidi zifanyike katika kipengele hichi ili kuona mfanano na tafauti miongoni mwa lahaja za Kiswahili kwa ujumla.
- ItemUlinganishi wa Njeo na Hali kaika Lahaje za Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) HAMAD, Salma OmarUtafiti huu umelenga kulinganisha uwakilishaji wa njeo na hali katika lahaja za Kipemba (KP), Kitumbatu (KT) na Kimakunduchi (KM) kwa kuzingatia maumbo ya vitenzi vya lahaja hizi. Lengo hili limefikiwa kwa kupitia malengo mahususi ambayo ni kubainisha mofimu za njeo na hali katika KP, kubainisha mofimu za njeo na hali katika KT, kubainisha mofimu za njeo na hali katika KM na kufafanua kufanana na kutafautiana kwa lahaja hizo katika uwakilishaji wa njeo na hali. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya utambuzi ya Guillaume (1965) na nadharia ya Fonolojia Zalishi ya Chomsky na Halle (1968). Data za utafiti huu zimekusanywa kwa mbinu ya kusoma maandiko, usaili na uchunguzi. Utafiti huu umebaini kwamba lahaja zote tatu zilizotafitiwa zina idadi sawa ya aina za njeo na hali. Katika uwakilishaji wa njeo na hali hizo, kuna baadhi ya maumbo ya mofimu yamefanana kwa lahaja zote tatu, baadhi yamefanana kati ya KM na KT na baadhi yamefanana kati ya KT na KP. Hata hivyo, tukiachana na maumbo ya mofimu yaliyofanana kwa lahaja zote tatu, hakujajitokeza umbo jingine lolote la mofimu lililofanana kati ya KM na KP. Hali hii inasababisha mfanano kuwa mkubwa kati ya KM na KT na pia kati ya KT na KP huku kukiwa na tafauti kubwa kati ya KM na KP katika vipengele hivi vya kimofosintaksia na kimofosintasematiki vya uwakilishaji wa njeo na hali. Mtafiti amependekeza tafiti zaidi zifanyike katika kipengele cha njeo na hali kwa lahaja zote za Kiswahili ili kubaini lahaja zipi zinafanana na zipi zinatafautiana miongoni mwa lahaja hizo. Aidha, kuna haja ya kutafiti kwa kina sababu ya mfanano na tafauti hizo.
- ItemUshikamano wa Sentesi katika Riwaya za Kiswahili: Ulinganishi wa Nyota Rehema na Utengano(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) ALI, Ziada HajiUshikamano ni dhana ya kisemantiki, ambayo hurejelea tabia au sifa za vipashio vikubwa zaidi ya mofimu, vinavyoambatanishwa pamoja katika sentensi ili kuunda matini. Dhana hii kwa muda mrefu imeonekana kama kuwa haiwezi kuangaliwa katika matini za fasihi, badala yake huangaliwa katika matini nyengine tu ambazo si za fasihi. Lengo la utafiti huu ni kuchunguza ushikamano wa kisarufi katika riwaya za Kiswahili, ikitolewa mifano kutoka katika riwaya za Nyota ya Rehema iliyoandikwa na Mohamed Suleiman Mohamed, mwaka 1976; na Utengano, iliyoandikwa na Said Ahmed Mohammed mwaka 1980. Data za utafiti huu zimepatikana kwa njia ya kudurusu riwaya hizo, na makala mbalimbali zilizosaidia kupatikana kwa data sahihi. Utafiti huu umebaini kuwa waandishi wa riwaya za Nyota ya Rehema na Utengano wametumia vijenzi vya ushikamano vya aina nne katika kazi zao. Vijenzi hivyo ni urejeleaji, udondoshaji, ubadilishaji na uunganishaji. Utafiti huu utasaidia kutoa mwangaza kwa watafiti kuchambua kazi za fasihi kwa kutumia vipengele mbalimbali vya kiisimu. Vilevile utasaidia kuwakumbusha waandishi kuwa isimu na fasihi ni taaluma zenye uhusiano wa karibu hivyo katika uandishi wao waangalie taaluma zote mbili wasiegemee upande mmoja.
- ItemAina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) MOH’D, Masoud NassorUtafiti huu wenye anuani: Aina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili umeangalia dhima za usambamba katika riwaya nne teule za Kiswahili; Nyota ya Rehema (1975), Kiu (1972), Ukiwa (1976) na Mafuta (1985). Mbinu ya usambamba ni moja wapo ya kipengele muhimu sana katika kazi mbalimbali za fasihi. Mbinu hii hutumiwa zaidi katika fasihi yenye mwelekeo wa kishairi kama vile mashairi na tenzi. Katika nathari mbinu hii imekuwa pia ikitumika lakini bila kupewa umuhimu unaostahiki kutoka kwa waandishi na wachamabuzi. Sio wachambuzi wengi walioshughulikia mbinu hii katika tahakiki zao. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza aina na dhima za usambamba katika riwaya teule za Kiswahili. Aidha mazingira ya kutokea kwa mbinu ya usambamba katika riwaya hizo pia yalichunguzwa. Data za msingi za utafiti huu zilikusanywa kutokana na udurusi wa riwaya teule na data za sekondari zilikuwa ni maoni ya wasailiwa zilizokusanywa kwa njia ya usaili, hojaji na majadiliano kimakundi.Utafiti uliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya umuundo iliyotumika kuangalia usambamba na aina zake na nadharia ya uamilifu ambayo imetumika kuangalia dhima za usambamba katika riwaya zilizochunguzwa. Uchunguzi umebaini kuwepo kwa aina mbalimbali za usambamba wenye dhima anuai. Aina hizo zilibainika kujitokeza katika mazingira maalumu katika matini.. Utafiti huu umekuwa na umuhimu mkubwa katika fasihi ya Kiswahili hasa kwa kuwa umetumia misingi ya kilughawiya kuichambua fasihi ya Kiswahili. Aidha pamepatikana utafiti umeibua mwamko juu ya kuvishughulikia vipengele vya kifasihi vilivyopuuzwa kwa muda mrefu. Baada ya utafiti huu, ipo haja ya kufanyika kwa tafiti nyingine za kiusambamba katika tanzu nyingine za fasihi andishi kama vile tamthilia na hadithi fupi.
- ItemUsasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) MOHAMED, Omar SalumUtafiti huu unahusu ‘Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa’. Mashairi ya nyimbo kadhaa wa kadhaa za taarab yamechunguzwa. Uchunguzi ulianzia na mashairi ya nyimbo za taarab halisi ambayo yametumika kama kigezo msingi katika kutambulisha usasa wa mashairi ya taarab ya sasa. Utafiti umefanyika katika wilaya tatu za Tanzania Visiwani na wilaya mbili za Tanzania Bara. Kwa upande wa visiwani ni Wilaya ya Chake Chake iliyopo Mkoa wa Kusini Pemba, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na Wilaya ya Mjini katika Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Kwa Bara, ni Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni, Daressalaam. Malengo ya utafiti huu yalikuwa matano. La kwanza, kuainisha sifa bainifu za mashairi ya taarab halisi. La pili ni kudhihirisha mambo yaliyobadilika katika mashairi ya taarab ya sasa. La tatu ni kupambanua sababu za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La nne, kutathmini athari za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La tano ni kuchunguza namna wasanii na wapenzi wa nyimbo za taarab wanavyoyapokea mabadiliko ya fani na maudhui yaliyomo kwenye mashairi ya taarab ya sasa. Data ilipatikana kupitia mbinu ya ushiriki nafsia, mbinu ya mahojiano, mbinu ya dodoso na mbinu ya kuwa na mtafiti msaidizi. Pamoja na mbinu hizo utafiti ulitumia Nadharia ya Uamilifu, Nadharia ya Semiotiki na Unadharia Unaozama, pamoja na Mkabala wa Utafsiriji wa Vitendo na Mkabala wa Kiislamu. Watafitiwa walikuwa watunzi wa mashairi, waimbaji, wapiga ala za muziki pamoja na washabiki/wapenzi wa muziki wa taarab. Uchambuzi wa data umeonesha kuwa ni kweli kabisa kwamba pana usasa wa waziwazi kwenye mashairi katika taarab ya sasa. Usasa huo ndio msingi uliyoshusha hadhi ya mashairi ya taarab ya sasa na kuwa maneno tu. Vile vile, muziki huo utambulikanao kama taarab ya sasa wakosa vigezo thabiti vyenye kuyakinisha uhalali wa kuitwa taarab.
- ItemDhima za Majina katika Nyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Kitumbatu(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) ALI, Khatibu HabibuUtafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza “Dhima za Majina katika Vyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Malengo mahsusi ya ufafiti huu yalikuwa kuchambua maana ya majina katika vyombo vya uvuvi, kuchunguza dhima za majina ya vyombo hivyp katika jamii husika, na kubainisha athari za majina ya vyombovya uvuvi kwa jamii yaTumbatu. Ili kufanikisha utafiti huu,nadharia ya Upokeaji na Semiotiki zilitumika, Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni pamoja na maktaba na mahojiano ya ana kwa ana. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha “Dhima za Majina katika Vyombovya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Mtokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, majina yamegawika katika makundi tofauti na kunasibishwa katika makundi hayo kulingana na maana yake kifasihi. Makundi hayo ni majazi, misimu, mafumbo jina, lakabu na mafumbo ya kiimani. Kwa upande wa dhima za majina hayo nipamoja nakutunza historia na matukio muhimu ya jamii, kutambulisha chombo katika taasisi rasmi, kudokeza wasifu wa chombo, nahodha na hata mmiliki wa chombo.Majina hayo yanaendeleza majina na kueleza fasihi pamoja na kujenga utani katika jamii. Na kwa upande wa athari; athari chanya ni kutumika katika usajili, kutofautisha chombo kimoja na kingine, kuendeleza vipawa vya wanajamii, kutumika kama ni dafina ya kuhifadhia matukio ya kijamii na mambo ya kihostoria. Na, athari hasi; majinahutumika kuendeleza chuki na uhasama baina ya wanajamii na kujenga mazingira ya hasada na mikosi juu ya chombo pamoja na kubomoa na kuchafuamaadili ya jamii husika.
- ItemMatumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili(SUZA, 2018-01-01) HAJI USSI, NADHRAUtafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika kukusanya data za maktabani, mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia makala mbalimbali zinazohusiana na utafit huu. Kwa upande wa data za uwandani, mtafiti alitumia mbinu ya usaili, hojaji na uchunguzi makinifu kwa kutumia usampulishaji mdokezo na lengwa. Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia mkabala wa kiidadi na mkabala stahilifu. Hata hivyo, mikabala yote ilitumika pale palipohitajika. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ilitumika kuchambulia data zinazohusiana malengo mahsusi ya utafiti huu na Nadharia ya Maana ni Matumizi ilitumika kuchambua data kwa pale panapostahiki. Matokeo ya utafiti huu, yaliweza kutupatia sifa tafauti za kiuzungumzaji katika maneno na mitindo ya sentensi katika kipengele cha sauti, maneno, sentensi na maana. Pia utokeaji wa lugha ya Kiswahili katika miktadha mbalimbali unatafautiana kimaana na kimuundo na unafafana katika utumiaji wa baadhi maneno na kwa upande wa kiisimu tuliweza kubaini changamoto hasi katika fonolojia, mofolojia, sintaksia na msamiati na chanya katika semantiki na msamiati, aidha kwa upande usio wa kiisimu tuliweza kupata changamoto hasi zaidi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mtafiti anapendekeza kuwa jamii itoe taaluma maalumu itakayoshughulikia kuthibiti na kuhifadhi matumizi sahihi ya lugha.
- ItemMATUMIZI YA LUGHA YA WAZEE WA KIKE NA ATHARI ZAKE KWA WATOTO ZANZIBAR(SUZA, 2018-01-20) HAFIDH, Zainab AliUtafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto.Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahil
- ItemUundaji wa Istilahi za Kiswaili: Mfano wa Istilahi za Sayansi ya Kumpyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(SUZA, 2018-10-01) SALEH KHALFAN, ALLYUtafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kupitia orodha za istilahi za uwanja huo pamoja na ujazaji wa dodoso na mahojiano ya kundi lengwa ambalo lilihusisha wataalamu na wanafunzi wa taaluma hizo. Imegundulika kwamba takriban asilimia 50 tu ya istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA zinazofahamika kwa watumiaji wake. Aidha, istilahi zinazokubalika kwa watumiaji ni asilimia 51. Hivyo, kuna uhusiano mkubwa kati ya kufahamika kwa istilahi na kukubalika kwake. Utafiti pia umegundua kwamba sababu zilizochangia kutokubalika kwa baadhi ya istilahi ni pamoja na maana ya istilahi hizo kuwa tafauti na maana ya asili katika Kiingereza, ugumu wa kufahamika kwa istilahi, kwenda kinyume na utamaduni wa Waswahili na kutopendwa na watumiaji. Kwa upande wa Mlango wa Lugha, imebainika kwamba baadhi ya istilahi zinakwenda kinyume na kanuni za kisarufi za miundo ya maneno ya Kiswahili, ikiwemo miundo ya silabi na maneno isiyokubalika kwa mujibu wa kanuni za Kiswahili.
- ItemMatumizi ya Kipashio "ni" katika Kitumbatu(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-11) HIJA, Silima HajiUtafiti huu unahusu matumizi ya kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Utafiti umefanywa katika Wilaya ya Kaskazini A, katika Wilaya ndogo ya Tumbatu, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zimepatikana kwa njia ya usaili, uchunguzi makini na masimulizi kutoka kwa wanafunzi na walimu wa Skuli za Sekondari za Tumbatu pamoja na wazee kutoka katika shehia ya Jongowe na Gomani. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za maneno ambazo huchukua kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Kufafanua mazingira ya utokeaji wa kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Kujadili dhima ya kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Nadharia ya Umuundo imetumika katika utafiti huu. Utafiti umeonesha kuwa kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu kina matumizi mbalimbali kwa watumiaji wa lahaja hiyo yaani Watumbatu. Miongoni mwa matumizi hayo ni kipashio ‘ni’ kama kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja mtenda na mtendwa, kielezi cha mahali, kiwakilisha cha tukio, mzizi wa neno wenye hadhi ya swali na kitenzi kishirikishi. Utafiti huu ni muhuimu kwa sababu unawasaidia walimu, wanafunzi na watafiti wa somo la lughawiya katika kupata marejeo.
- ItemUchambuzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar:(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-11) HAJI, Hassan GoraKazi hii inahusu Uchambuzi wa Nyimbo za Uganga wa Pepo Zanzibar: Mtindo na Dhima zake (mfanokutoka jamii ya Watumbatu). Katika tasnia hii nyimbo za uganga wa pepo wa aina tatu zilikusanywa na kuchambulia. Nyimbo hizi ni za uganga wa pepo wa maruhani, rubamba, na puuwo. Utafiti huu ilifanywa katika vijiji vya Chaani Masingini, Mkwajuni, Kibeni na Tumbatu Kichagani. Katika maeneo hayo uganga ulihusika unafanywa sana na wakaazi wake. Lengo kuu la utafifi huu lilikua ni kufanya uchambuzi wa mtindo na dhima wa nyimbo za uganga wa pepo. Waganga, wari na wataalamu wa fasihi ya Kiswahili walitumiwa kutoa taarifa juu ya uganga na nyimbo zake. Watoa taarifa hawa walikua wazee na vijna – Wanawake na wanaume. Katika uchambuzi, tulichambua vipengele vya mtindo wa nyimbo za uganga wa pepo kwa kutumia njia ya maelezo. Tulitumia mbinu ya umakinifu (ushuhudiaji) na mahusiano au usaili katika kukusanya data za utafiti. Aidha katika uchambuzi wa nyimbo za uganga wa pepo tulitumia nadharia za muundo, dhima na kazi. Nadaria hizi zilifanikisha sana katika kusaidia uchambuzi wa nyimbo hizo. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa nyimbo za uganga wa pepo zimetungwa na kuimbwa kwa kutumia vipengele vya matumizi ya maneno, takriri neno, anaphora, epifora, tasai, taksila, tasako, tempo na sauti, usamamba, tanakuzi, mtindo wa nyimbo huru, mtindo wa kutumia mshororo mmoja, na mtindo wa kupokezana katika uimbaji. Kila mtindo ulikua na dhima zake kama vile kusisitiza jambo, kuvutia hadhira, kudokeza asili ya wimbo na kufanya wimbo kuimbika na kuhifadhika kwa uhalisia. Aidha tulibaini kuwa nyimbo hizi zilikua na dhima mbali mbali kama vile kubembeleza, kujuvya, kuchombeza na kuhamasisha.
- ItemVitendoneni Katika Hutuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka 2015, na Athari zake kwa Wanajamii wa Zanzibar(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-12) HAJI, Mahmoud YussufUtafiti huu Umechunguza Vitendoneni Katika Hotuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka, 2015 na Athari Zake kwa Wanajamii wa Zanzibar. Huu ni utafiti wa uwandani uliojumuisha matumizi ya mbinu shirikishi, usaili na maktabani katika kukusanya data na hatimaye data zimechambuliwa kwa njia ya kimaelezo na kitakwimu. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa. 1) Kubainisha vitendoneni vinavyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. 2) Kuchambua nia na nguvu za tamko kwa wazungumzaji kwenda kwa hadhirawanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. 3) Kuchambua athari hasi na chanya za vitendoneni kwa wanajamii wanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Kitendoneni iliyoasisiwa na Austin, (1962) pamoja na Nadharia ya Umaanishiiliyoasisiwa na Grice (1975). Jumla ya vitendoneni athari vilikuwa, 120 ambapo vitendoneni vyenye mwelekeo chanya ni 90 ikiwa sawa na 75% na vitendoneni vyenye mwelekeo hasi ni 30 ikiwa sawa na 25%. Imegundulika kuwa vitendoneni vilivyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguzi vina athari chanya na athari hasi kwa hadhira. Utafiti huu umeonesha kuwa, baadhi ya wazungumzaji wanatumia vitendoneni vinavyokiuka utaratibu wa mazungumzo na baadhi yake wanatumia vitendoneni vinavyozingatia utaratibu wa mazungumzo. Aidha imebainika kuwa yapo matamko ndani yake zimo kauli zisizokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Vile vile yapo matamko ambayo ndani yake zimo kauli zinazokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Mbali na hayo, wamekuwepo wazungumzaji wanaozingatia muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira na wanaokiuka muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira kiasi ya kuchangia mawazo yenye mtazamo hasi na mawazo yenye mtazamo chanya kwa hadhira. Pia imebainika kuwa yapo matamko ya hotuba ambayo ndani yake yanatumia kanuni za ushirikiano pamoja na kanuni za unyenyekevu.
- ItemNafasi ya Kasida za Kiswahili Katika Kumtetea Mwanamke Zanzibar(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-12) HAMAD, Kombo SharifUtafiti huu umeshughulikia nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Kiini cha utafiti kimetokana na dhana kwamba baadhi ya watu katika jamii wanaamini kuwa kasida za Kiswahili hazina mchango wowote kwa jamii zaidi ya kuburudisha. Kutokana na hali hiyo, mtafiti alipata wazo la kufanya kazi hii baada ya kubaini kuwa hakuna utafiti wowote uliofanywa ukizihusisha kasida za Kiswahili katika utetezi wa mwanamke. Hivyo, utafiti huu umebainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili. Utafiti huu una lengo kuu moja ambalo ni kuchunguza nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Lengo hilo limekamilishwa na malengo mahsusi ambayo ni kubainissha kasida za Kiswahili zinazomtetea mwanamke, kubainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili na kutathmini nafasi ya kasida za Kiswahili kwa jamii ya wanawake . Dira iliyotumika kuongoza utafiti huu ni nadhariya ya ufeministi wa Kiislamu. Mbinu za utafiti zilizotumika katika kazi hii, ni pamoja na mbinu ya maktabani, uwandani, mbinu za mahojiano ya ana kwa ana na watafitiwa na mbinu ya uchunguzi shirikishi uliofanywa katika sehemu ambazo kasida huwasilishwa. Utafiti umebainisha kuwa zipo baadhi ya kasida za Kiswahil zenye utetezi wa mwanamke. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwepo kwa utetezi wa mwanamke katika nyanja za kijamii, kielimu, kiuchumi na kisiasa. Utafiti umebaini kuwa, kasida zinamtetea mwanamke zaidi katika suala la ndoa. Utetezi wa mwanamke uliobainika katika kasida ni pamoja kuthaminiwa idhini ya mwanamke katika ndoa. Na mwanamke kupewa nafasi ya kuchagua mchumba
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »