Uhalisia wa Utabaka katika Tamthilia ya Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga

No Thumbnail Available
Date
2018-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Tamthiliya za Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga zimepata umaarufu na kuwa tamthiliya nzuri na imara za mtunzi Khamis. Utafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza uhalisia wa utabaka katika tamthiliya mbili (Janga la Warevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga). Malengo mahsusi ya ufafiti huu yalikuwa ni, kuchambua uhalisia wa utabaka katika kazi za Khamis, na Kuonesha athari inayoipata jamii kutokana na utabaka unaozungumzwa na Khamis. Ili kufanikisha utafiti huu Nadharia mbili zilitumika, Nadharia ya Umaks na Nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa. Nadharia ya Umaks ilisaidia kufafanua aina za utabaka katika kazi za tamthiliya za Khamis, na nadharia ya Uhalisia wa Kijamaa nayo ilitumika kuchambua athari za utabaka katika jamii. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni maktaba. Data zilizokusanywa zimechambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha hali halisi ya Utabaka katika jamii. Mtokeo ya utafiti yanaonesha kwamba utabaka unaojitokeza zaidi katika tamthiliya za Janga la Werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga ni utabaka wa kiuchumi, kisiasa, kiitikadi na utabaka wa hali na hadhi. Athari zilizobainika ni kuibuka kwa migogoro katika jamii, umasikini, ufisadi, ukiukwaji wa haki katika jamii na utafutaji wa haki kwa nguvu ya umma.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Utabaka kaika tamthilia - Janga la werevu na Kitumbua Kimeingia Mchanga 2. Athari za utabaka - Tamthilia
Citation