Udondoshaji katika Lahaja za Kipemba

No Thumbnail Available
Date
2018-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu umelenga kuchunguza udondoshaji katika lahaja za Pemba. Lengo hili limefikiwa kwa kupitia malengo mahususi ambayo ni kubainisha aina za udondoshaji katika lahaja za Pemba, kufafanua mazingira ya utokeaji wa udondoshaji katika lahaja za Pemba na kubainisha kategoria za maneno ambazo hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Nadharia zilizotumika kuongoza utafiti huu ni nadharia ya Umuundo na nadharia Jumuishi. Kwa upande wa nadharia ya Umuundo, msingi wake mkuu ni kuwa mfumo lugha ni mfumo changamano ambapo ndani yake kuna mifumo mengine tafauti yenye kuhusiana inayoanzia katika kiwango cha sauti, mofimu, neno, virai, vishazi, sentensi, hadi kufikia mshikamano wa sentensi na maana. Msingi mkuu wa nadharia Jumuishi ni kuwa jamiilugha inajengwa na wale watu wanaojiona na kutambua wenyewe kuwa wao wanatokana na jamiilugha moja, ambayo iko tafauti na jamiilugha nyengine. Data za utafiti huu zimepatikana kwa njia ya kusoma maandiko, usaili, uchunguzi makini, uchunguzi shirikishi na usimulizi. Utafiti huu umebaini kwamba kuna aina nne za udondoshaji katika lahaja za Pemba. Aidha udondoshaji katika lahaja za Pemba hutokea katika mazingira tafauti. Data zimeonesha kuwa aina saba za maneno hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Mtafiti amependekeza tafiti zaidi zifanyike katika kipengele hichi ili kuona mfanano na tafauti miongoni mwa lahaja za Kiswahili kwa ujumla.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Lahaja za Kipemba
Citation