Udondoshaji katika Lahaja za Kipemba

dc.contributor.authorABDALLA, Maryam Msabah
dc.date.accessioned2020-08-18T08:09:37Z
dc.date.available2020-08-18T08:09:37Z
dc.date.issued2018-01
dc.descriptionAvailable in print form, Tunguu Reference Libraryen_US
dc.description.abstractUtafiti huu umelenga kuchunguza udondoshaji katika lahaja za Pemba. Lengo hili limefikiwa kwa kupitia malengo mahususi ambayo ni kubainisha aina za udondoshaji katika lahaja za Pemba, kufafanua mazingira ya utokeaji wa udondoshaji katika lahaja za Pemba na kubainisha kategoria za maneno ambazo hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Nadharia zilizotumika kuongoza utafiti huu ni nadharia ya Umuundo na nadharia Jumuishi. Kwa upande wa nadharia ya Umuundo, msingi wake mkuu ni kuwa mfumo lugha ni mfumo changamano ambapo ndani yake kuna mifumo mengine tafauti yenye kuhusiana inayoanzia katika kiwango cha sauti, mofimu, neno, virai, vishazi, sentensi, hadi kufikia mshikamano wa sentensi na maana. Msingi mkuu wa nadharia Jumuishi ni kuwa jamiilugha inajengwa na wale watu wanaojiona na kutambua wenyewe kuwa wao wanatokana na jamiilugha moja, ambayo iko tafauti na jamiilugha nyengine. Data za utafiti huu zimepatikana kwa njia ya kusoma maandiko, usaili, uchunguzi makini, uchunguzi shirikishi na usimulizi. Utafiti huu umebaini kwamba kuna aina nne za udondoshaji katika lahaja za Pemba. Aidha udondoshaji katika lahaja za Pemba hutokea katika mazingira tafauti. Data zimeonesha kuwa aina saba za maneno hupata udondoshaji katika lahaja za Pemba. Mtafiti amependekeza tafiti zaidi zifanyike katika kipengele hichi ili kuona mfanano na tafauti miongoni mwa lahaja za Kiswahili kwa ujumla.en_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/149
dc.language.isootheren_US
dc.publisherThe State University of Zanzibar (SUZA)en_US
dc.subject1. Lahaja za Kipembaen_US
dc.titleUdondoshaji katika Lahaja za Kipembaen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
LAHAJA ZA KIPEMBA.pdf
Size:
827.19 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: