Dhamira Zijengwazo na Taswira katika Methali za Wapemba
No Thumbnail Available
Date
2017-12
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu umechunguza dhamira zijengwazo na taswira katika methali za Kiswahili. Chimbuko la tatizo la utafiti huu lilikuwa ni kutoshughulikiwa na watafiti suala la taswira katika ujenzi wa dhamira katika methali za Wapemba. Kwa hivyo, utafiti huu umeweza kubainisha matumizi hayo kwa kuonesha taswira mbalimbali ambazo zimesaidia kujenga dhamira kwa jamii ya Wapemba.
Mtafiti amekuwa na lengo kuu moja na malengo mahsusi matatu ambayo yote yamemsaidia kugundua taswira mbalimbali zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kuzijenga dhamira za methali hizo. Mtafiti alitumia data za uwandani na aliweza kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni pamoja na wazee, wanafunzi na walimu wa somo la Fasihi ya Kiswahili wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Wete Pemba. Utafiti huu ulitumia machapisho tofauti yakiwemo vitabu na majarida. Data za msingi kwa kuhojiana na watafitiwa ana kwa ana na data fuatizi zimepatikana kutoka maktabani na kwenye mtandao. Nadharia za Uamilifu na Umuundo umetumika katika utafiti huu.
Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa methali zimejengwa vizuri na taswira ambazo zimeibua dhamira zilizokamilika. Methali ambazo zimechunguzwa ni pamoja na zile ambazo zimegawiwa kitaswira kimakundi kwa mujibu wa Khatib (2014), kama ifuatavyo: Kizuolojia, kibotania, kijiolojia, kiastronomia, kiteolojia na taswira za vitu vya kawaida. Aidha, matokeo hayo ya uafiti pia yamebainisha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya taswira zijengazo dhamira katika maisha ya jamii ya Wapemba. Kwa vile methali ndiyo hazina kuu ambayo jamii inaitumia hasa wazee kwa kutoa maadili ya jamii, bado jamii ina nafasi yake kuzitumia methali katika maisha yao ambayo ni njia muhimu ya kuwafundishia watoto ambao ndiyo taifa la kesho. Hivyo methali zinahitajiwa zitumiwe kwa kuangalia mjengeko wake wa maneno ambayo ndiyo hubeba taswira zenye lengo maalumu
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library