Muundo wa Lugha Katika Maishairi ya Watungaji Wateule wa Zanzibar
No Thumbnail Available
Date
2017-11
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar
Abstract
Utafiti huu unahusu “Muundo wa Lugha katika Mashairi ya Watungaji Wateule wa
Zanzibar”. Diwani nne za watungaji wawili wa Zanzibar zilichambuliwa. Diwani
hizo ni Kina cha Maisha ya Mohamed (1984) na Jicho la Ndani ya Mohamed
(2002). Diwani nyengine ni Andamo iliyoandikwa na Ghassani (2016a) na Siwachi
Kusema pia ya Ghassani (2016b). Utafiti huu ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi
A, Magharibi B na Wilaya ya Kusini, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zilipatikana
kwa njia ya maktaba, usaili kwa wahakiki wa fasihi na hojaji kwa wanafunzi wa
vyuo vikuu vya Zanzibar. Njia ya maktaba iliwezesha kupata data nyingi za msingi
zilizotimiza malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuchunguza vijenzi vya lugha
katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki, vilivyoyajenga mashairi
ya watungaji wateule wa Zanzibar kimaana na kiujumi. Aidha, utafiti ulichunguza
ukiushi wa kanuni za kisarufi katika mashairi hayo na jinsi vijenzi vya lugha
vilivyopambanua mtindo. Nadharia ya Umuundo na Umuundoleo zilitumika katika
uchambuzi wa data. Utafiti umeonesha kuwa watunzi wote wamevitumia vijenzi vya
lugha katika ngazi ya fonolojia, mofolojia, sintaksia na semantiki kuyajenga
mashairi yao. Watunzi wote wamevitumia vijenzi vya lugha kwa kuzingatia kanuni
za lugha kwa usahihi kulingana na muktadha, mazingira na wakati. Aidha,
wamevisarifu vijengo vya lugha kuimarisha sanaa zao kiujumi na kimaana kwa
kuzingatia sifa za lugha ya kishairi inayoendana na mkwepo wa sarufi. Hali hiyo
imedhihirisha kuwa upo ufungamanifu kati ya vijenzi vya kimuundo na ushairi, kwa
kuwa vijenzi hivyo ndivyo vilivyotumika kuyajenga mashairi ya watungaji wateule
wa Zanzibar.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library and Global Center
Keywords
Mashairi, Muundo wa Lugha -Mashairi
Citation
Asha Mhene Hamad