Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Title
Now showing 1 - 20 of 54
Results Per Page
Sort Options
- ItemAina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) MOH’D, Masoud NassorUtafiti huu wenye anuani: Aina za Usambamba na Dhima zake katika Riwaya Teule za Kiswahili umeangalia dhima za usambamba katika riwaya nne teule za Kiswahili; Nyota ya Rehema (1975), Kiu (1972), Ukiwa (1976) na Mafuta (1985). Mbinu ya usambamba ni moja wapo ya kipengele muhimu sana katika kazi mbalimbali za fasihi. Mbinu hii hutumiwa zaidi katika fasihi yenye mwelekeo wa kishairi kama vile mashairi na tenzi. Katika nathari mbinu hii imekuwa pia ikitumika lakini bila kupewa umuhimu unaostahiki kutoka kwa waandishi na wachamabuzi. Sio wachambuzi wengi walioshughulikia mbinu hii katika tahakiki zao. Lengo la utafiti huu lilikuwa kuchunguza aina na dhima za usambamba katika riwaya teule za Kiswahili. Aidha mazingira ya kutokea kwa mbinu ya usambamba katika riwaya hizo pia yalichunguzwa. Data za msingi za utafiti huu zilikusanywa kutokana na udurusi wa riwaya teule na data za sekondari zilikuwa ni maoni ya wasailiwa zilizokusanywa kwa njia ya usaili, hojaji na majadiliano kimakundi.Utafiti uliongozwa na nadharia mbili; nadharia ya umuundo iliyotumika kuangalia usambamba na aina zake na nadharia ya uamilifu ambayo imetumika kuangalia dhima za usambamba katika riwaya zilizochunguzwa. Uchunguzi umebaini kuwepo kwa aina mbalimbali za usambamba wenye dhima anuai. Aina hizo zilibainika kujitokeza katika mazingira maalumu katika matini.. Utafiti huu umekuwa na umuhimu mkubwa katika fasihi ya Kiswahili hasa kwa kuwa umetumia misingi ya kilughawiya kuichambua fasihi ya Kiswahili. Aidha pamepatikana utafiti umeibua mwamko juu ya kuvishughulikia vipengele vya kifasihi vilivyopuuzwa kwa muda mrefu. Baada ya utafiti huu, ipo haja ya kufanyika kwa tafiti nyingine za kiusambamba katika tanzu nyingine za fasihi andishi kama vile tamthilia na hadithi fupi.
- ItemAssessing Strategies of Reducing School Dropout in Zanzibar(THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR, 2019-11) Ali, Mwajuma AbdallahThis study investigated effectiveness of strategies that reduce school dropout in upper primary and lower secondary students in Zanzibar, the case of Central District. Specifically this study focused on factors that cause school dropout, strategies designed to reduce dropout problem and relevance of strategies that were designed to reduce school dropout. The study adopted qualitative approach targeting upper primary and lower secondary levels of students in Unguja Ukuu, Kibele, Kikungwi and Tunguu schools in Central District. Sample sizes of 55 respondents used by using purposive sampling and convenience sampling procedures. Interview and focus group discussion methods used to collect data. Interview and focus group data were recorded by using mobile sound recorder. Collected data were coded and analyzed thematically. The study revealed factors for school dropout in upper primary and lower secondary level comprised of school related factors as well as out of school ones. The former include ineffective ways of teaching, students’ class repetition, lack of school feeding programme and students’ embarrassment. The latter embrace economic related factors, social related factors, geographical factors and individual factors. The study discovered several strategies have been designed to reduce school dropout, including establishment of guidance and counseling units, use of police stations as well as use of alternative punishments. The study concluded some strategies that are in place have had little success because they are not practiced effectively and through their application they fail to reduce school dropout while strategies have had success because they are practiced effectively as well as they flourished to reduce dropouts. The study recommends that emphasizes should put much to the uses of those effective strategies that help to reduce school dropout, there is a need to emphasize on the use of effective strategies that are in place, schools to improve strong relationship between parents and teachers so as to keep students present and active in schools, as well as school should amend those ineffective strategies that are in place in order to increase the strategies which can help to reduce school dropout
- ItemCHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI KATIKA STADI YA KUSOMA(SUZA, 2019-12-12) KHALFAN, Shani SuleimanLengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza changamoto zinazowakabili walimu katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Stadi ya Kusoma. Utafiti huu umefanywa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Kituo cha Kiswahili na Utamaduni (KIU) katika tawi lake la Zanzibar. Mtafiti alitumia nadharia ya stadi ya kusoma ya Schema iliyoasisiwa na Barlett (1932) na kuungwa mkono na Rumelhart na Ortony (1977). Washiriki wa utafiti huu walikuwa ni walimu wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Zanzibar, Idara ya Kiswahili kwa Wageni na Kituo cha Kiswahili na Utamaduni. Mbinu za ukusanyaji data alizotumia mtafiti katika utafiti huu ni dodoso, usaili na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa walimu wanakabiliwa na changamoto nyingi katika ufundishaji wa stadi ya kusoma; kama ukosefu wa vifaa vya kufundishia, walimu kukosa mbinu za kisasa katika ufundishaji na ugumu wa matini zinazotumika kufundishia stadi ya kusoma. Changamoto hizo zimesababisha walimu kuumia muda mwingi katika ufundishaji, kutofikia malengo ya ufundishaji waliyojiwekea, kukosa ari, hamu na shauku ya kuendelea kufundisha na kutumia nguvu za ziada. Utafiti huu umetoa apendekezo kuwa ili ufundishaji wa stadi ya kusoma uwe na ufanisi, taasisi husika zinapaswa kutoa mafunzo ya mara wa mara kwa walimu, uandaaaji wa vifaa vya kisasa vya ufundishaji vinavyokwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia ya ufundishaji lugha. Walimu wajijengee tabia ya kujisomea na kujifunza kupitia mitandao badala ya kusubiri nafasi za ufadhili.
- ItemDhamira Zijengwazo na Taswira katika Methali za Wapemba(The State University of Zanzibar (SUZA), 2017-12) KHATIB, Time OmarUtafiti huu umechunguza dhamira zijengwazo na taswira katika methali za Kiswahili. Chimbuko la tatizo la utafiti huu lilikuwa ni kutoshughulikiwa na watafiti suala la taswira katika ujenzi wa dhamira katika methali za Wapemba. Kwa hivyo, utafiti huu umeweza kubainisha matumizi hayo kwa kuonesha taswira mbalimbali ambazo zimesaidia kujenga dhamira kwa jamii ya Wapemba. Mtafiti amekuwa na lengo kuu moja na malengo mahsusi matatu ambayo yote yamemsaidia kugundua taswira mbalimbali zilizosaidia kwa kiasi kikubwa kuzijenga dhamira za methali hizo. Mtafiti alitumia data za uwandani na aliweza kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni pamoja na wazee, wanafunzi na walimu wa somo la Fasihi ya Kiswahili wa Skuli za Sekondari za Wilaya ya Wete Pemba. Utafiti huu ulitumia machapisho tofauti yakiwemo vitabu na majarida. Data za msingi kwa kuhojiana na watafitiwa ana kwa ana na data fuatizi zimepatikana kutoka maktabani na kwenye mtandao. Nadharia za Uamilifu na Umuundo umetumika katika utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwa methali zimejengwa vizuri na taswira ambazo zimeibua dhamira zilizokamilika. Methali ambazo zimechunguzwa ni pamoja na zile ambazo zimegawiwa kitaswira kimakundi kwa mujibu wa Khatib (2014), kama ifuatavyo: Kizuolojia, kibotania, kijiolojia, kiastronomia, kiteolojia na taswira za vitu vya kawaida. Aidha, matokeo hayo ya uafiti pia yamebainisha kuwa upo uhusiano mkubwa kati ya taswira zijengazo dhamira katika maisha ya jamii ya Wapemba. Kwa vile methali ndiyo hazina kuu ambayo jamii inaitumia hasa wazee kwa kutoa maadili ya jamii, bado jamii ina nafasi yake kuzitumia methali katika maisha yao ambayo ni njia muhimu ya kuwafundishia watoto ambao ndiyo taifa la kesho. Hivyo methali zinahitajiwa zitumiwe kwa kuangalia mjengeko wake wa maneno ambayo ndiyo hubeba taswira zenye lengo maalumu
- ItemDhima za Majina katika Nyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Kitumbatu(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) ALI, Khatibu HabibuUtafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza “Dhima za Majina katika Vyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Malengo mahsusi ya ufafiti huu yalikuwa kuchambua maana ya majina katika vyombo vya uvuvi, kuchunguza dhima za majina ya vyombo hivyp katika jamii husika, na kubainisha athari za majina ya vyombovya uvuvi kwa jamii yaTumbatu. Ili kufanikisha utafiti huu,nadharia ya Upokeaji na Semiotiki zilitumika, Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni pamoja na maktaba na mahojiano ya ana kwa ana. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha “Dhima za Majina katika Vyombovya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Mtokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, majina yamegawika katika makundi tofauti na kunasibishwa katika makundi hayo kulingana na maana yake kifasihi. Makundi hayo ni majazi, misimu, mafumbo jina, lakabu na mafumbo ya kiimani. Kwa upande wa dhima za majina hayo nipamoja nakutunza historia na matukio muhimu ya jamii, kutambulisha chombo katika taasisi rasmi, kudokeza wasifu wa chombo, nahodha na hata mmiliki wa chombo.Majina hayo yanaendeleza majina na kueleza fasihi pamoja na kujenga utani katika jamii. Na kwa upande wa athari; athari chanya ni kutumika katika usajili, kutofautisha chombo kimoja na kingine, kuendeleza vipawa vya wanajamii, kutumika kama ni dafina ya kuhifadhia matukio ya kijamii na mambo ya kihostoria. Na, athari hasi; majinahutumika kuendeleza chuki na uhasama baina ya wanajamii na kujenga mazingira ya hasada na mikosi juu ya chombo pamoja na kubomoa na kuchafuamaadili ya jamii husika.
- ItemDHIMA ZA TAHARUKI KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI:(SUZA, 2019-12-01) HAMAD, Aminia HassanUtafiti huu umechunguza dhima za taharuki katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale na Kisima cha Giningi zilizotungwa na Muhammed Said Abdulla. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Data zake za msingi zimepatikana kwa njia ya maktaba, usaili kwa walimu na mahojiano kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Njia ya maktaba ilimuwezesha mtafiti kusoma riwaya zilizoteuliwa na kupata data za msingi ambazo zilitumika katika uchanganuzi. Data nyingine zilizopatikana kwa njia ya usaili na mahojiano zimetumika kutilia mkazo na kuzihakikisha data zilizopatikana kwa njia ya maktaba katika kufikiwa malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuainisha aina za taharuki, kufafanua mazingira ya utokeaji wake na kuelezea dhima zake. Matokeo ya utafiti yamebainisha aina za taharuki, mazingira yake na dhima zake, kwa kuongozwa na Nadharia ya Umuundo na Nadharia ya Uamilifu. Nadharia ya Umuundo imesaidia kuangalia aina za taharuki; taharuki msingi, taharuki ndogo na taharuki hamasishi na mazingira yake. Nadharia ya Uamilifu imetumika kuangalia dhima zake. Utafiti umeonesha kuwa ipo haja ya kuchunguzwa tena kipengele hiki cha taharuki katika tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili
- ItemDhima za Taharuki katika Riwaya za Kiswahili: Kisima cha Giningi ma Mzimu wa Watu wa Kale(SUZA, 2019-12-01) HASSAN HAMAD, AMINIAUtafiti huu umechunguza dhima za taharuki katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale na Kisima cha Giningi zilizotungwa na Muhammed Said Abdulla. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Data zake za msingi zimepatikana kwa njia ya maktaba, usaili kwa walimu na mahojiano kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Njia ya maktaba ilimuwezesha mtafiti kusoma riwaya zilizoteuliwa na kupata data za msingi ambazo zilitumika katika uchanganuzi. Data nyingine zilizopatikana kwa njia ya usaili na mahojiano zimetumika kutilia mkazo na kuzihakikisha data zilizopatikana kwa njia ya maktaba katika kufikiwa malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuainisha aina za taharuki, kufafanua mazingira ya utokeaji wake na kuelezea dhima zake. Matokeo ya utafiti yamebainisha aina za taharuki, mazingira yake na dhima zake, kwa kuongozwa na Nadharia ya Umuundo na Nadharia ya Uamilifu. Nadharia ya Umuundo imesaidia kuangalia aina za taharuki; taharuki msingi, taharuki ndogo na taharuki hamasishi na mazingira yake. Nadharia ya Uamilifu imetumika kuangalia dhima zake. Utafiti umeonesha kuwa ipo haja ya kuchunguzwa tena kipengele hiki cha taharuki katika tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili.
- ItemKAULI ZA NASAHA KATIKA HARUSI ZINAVYOJENGA UHUSIANO WA WANANDOA:(SUZA, 2021-12-01) BIROLI,FATMA YAKOUTUtafiti huu ulikuwa na lengo la kuchunguza kauli za nasaha katika harusi za Wapemba jinsi zinavyojenga uhusiano wa wanandoa. Utafiti ulikuwa na malengo mawili: Kuainisha kauli za nasaha anazopewa biharusi na bwanaharusi kwa mujibu wa utamaduni wa jamii ya Wapemba na kufafanua uhusiano wa ndoa unaojengwa na kauli hizo. Utafiti uliongozwa na nadharia ya uchambuzi makini wa matini. Utafiti ulifanyika katika wilaya mbili, Chake chake na Mkoani. Data zilikusanywa kupitia mbinu ya dodoso, usaili na ushuhudiaji. Sampuli ya watafitiwa thelathini (30) ilitumika. Utafiti umebaini kuwa kauli za nasaha zitolewazo katika harusi za Wapemba. Ziko kauli za nasaha ambazo zimefanana na zinajenga uhusiano baina ya biharusi na bwanaharusi katika maisha ya ndoa. Mfano “Jihadhari sana, usimruhusu mke kuwa na marafiki wengi na kutumia muda mwingi nje kwa kukaa na marafiki zake.” “Tahadhari sana na ulimi, tunakunasihi, ulimi wako unatakiwa utumie vizuri.” Pia mtafiti amegundua kauli za nasaha zimefanikiwa kuonesha uhusiano unaojengwa na kauli hizo kwa bwanaharusi na biharusi. Mfano wa kauli za nasaha zinazojenga uhusiano kwa bwanaharusi na biharusi: “Tunakunasihi, mke ni mkeo, ndio mwenzio usimfanyie jeuri wala dharau.” “Zingatia vizuri tunayokunasihi, umuheshimu mumeo umuone ni mumeo wala simdharau.” Mtafiti anapendekeza kuwa kauli za nasaha ziendelee kutumika katika jamii ya Wapemba na jamii nyengine za Waswahili. Pia mtafiti anapendekeza uchunguzi zaidi ufanyike katika uwanja wa kitaaluma utakaohusisha kauli za nasaha katika miktadha tafauti ikiwemo msibani, maofisini, mashuleni na miktadha mengineo ili kuzijenga jamii kuwa na maadili bora katika sehemu zote napokuwepo. Pia mtafiti anapendekeza watafiti wengine waangalie kauli za nasaha walizopewa wanandoa wakongwe na wanandoa wa sasa halafu walinganishe wepi waliofanikiwa kudumu katika ndoa zao.
- ItemKIRAI NOMINO KATIKA KIPEMBA: UCHANGANUZI WA KIMUUNDO(SUZA, 2019-09-01) JUMA, Bikombo FakiUtafiti huu umechunguza virai nomino katika Kipemba. Uchanganuzi wa kimiundo na umegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unajumuisha vipengele vya awali vya utafiti.Vipengele vilivyoelezwa katika sura ya kwanza ni usuli wa tatizo, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mipaka ya utafiti.Sura ya pili imeeleza mapitio ya machapisho na kiunzi cha nadharia, ambapo imetumika nadhari ya Sarufi jumuishi miundo virai (19). Aidha, sura ya tatu imejadili mbinu na njia za utafiti, vifaa vya utafiti, ukusanyaji wa data na uwasilishaji wa data. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni usaili, uchunguzi makini na hojaji. Sura ya nne imehusiana wa uchambuzi wa data ambao ulihusisha malengo matatu, ambapo lengo la kwanza ni ubainishaji wa miundo ya virai nomino katika Kipemba. Lengo la pili ni kufafanua utokeaji wa miundo ya virai nomino katika Kipemba. Na lengo la tatu ni kuchambua miundo ya virai nomino katika Kipemba kwa mujibu wa nadharia iliyotumika katika utafiti huu ambayo ni Sarufi jumuishi muundo virai. Sura ya tano inaelezea matokeo ya utafiti huu, ambapo Kipemba kinaonesha kuwa kina miundo ya virai nomino ambayo inaonesha muunganiko wa nomino na viwakilishi au nomino na vivumishi ambapo husimama pamoja na kuunda tungo kirai. Vivumishi hivyo huweza kushikana na nomino au viwakilishi na huanzia na kimoja, viwili hadi vitatu
- ItemKIRAI NOMINO KATIKA KIPEMBA: UCHANGANUZI WA KIMUUNDO(SUZA, 2019-09-01) FAKI JUMA, BIKOMBOUtafiti huu umechunguza virai nomino katika Kipemba. Uchanganuzi wa kimiundo na umegawanywa katika sura tano. Sura ya kwanza ni utangulizi ambao unajumuisha vipengele vya awali vya utafiti.Vipengele vilivyoelezwa katika sura ya kwanza ni usuli wa tatizo, malengo ya utafiti, maswali ya utafiti, umuhimu wa utafiti na mipaka ya utafiti.Sura ya pili imeeleza mapitio ya machapisho na kiunzi cha nadharia, ambapo imetumika nadhari ya Sarufi jumuishi miundo virai (19). Aidha, sura ya tatu imejadili mbinu na njia za utafiti, vifaa vya utafiti, ukusanyaji wa data na uwasilishaji wa data. Mbinu zilizotumika katika utafiti huu ni usaili, uchunguzi makini na hojaji. Sura ya nne imehusiana wa uchambuzi wa data ambao ulihusisha malengo matatu, ambapo lengo la kwanza ni ubainishaji wa miundo ya virai nomino katika Kipemba. Lengo la pili ni kufafanua utokeaji wa miundo ya virai nomino katika Kipemba. Na lengo la tatu ni kuchambua miundo ya virai nomino katika Kipemba kwa mujibu wa nadharia iliyotumika katika utafiti huu ambayo ni Sarufi jumuishi muundo virai. Sura ya tano inaelezea matokeo ya utafiti huu, ambapo Kipemba kinaonesha kuwa kina miundo ya virai nomino ambayo inaonesha muunganiko wa nomino na viwakilishi au nomino na vivumishi ambapo husimama pamoja na kuunda tungo kirai. Vivumishi hivyo huweza kushikana na nomino au viwakilishi na huanzia na kimoja, viwili hadi vitatu
- ItemKiwango cha ukubalifu wa Istilahi za Kiswahili za Technolojia ya Habari na Mawasiliano Zanzibar :(The State University of Zanzibar (SUZA), 2017-11) IBRAHIM, Ulfat AbdulazizUtafiti huu unahusu “Kiwango cha ukubalifu wa istilahi za kiswahili za Teknolojia ya habari na mawasiliano, Zanzibar: mfano kutoka istilahi za Kilinux”. Utafiti huu umejikita katika kuchunguza mambo matatu ambayo: Mosi, kuelezea ukubalifu wa istilahi za TEHAMA zilizoundwa chini ya mradi wa Kilinux miongoni mwa Wazanzibari. Pili kufafanua matumizi halisi ya istilahi za Kiswahili za TEHAMA kwa watumiaji walioko katika sekta ya elimu Zanzibari. Tatu kubainisha endapo kuna istilahi nyingine za TEHAMA zinazotumika zisizo za Kilinux. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Istilahi za Kisayansi (NIK) iliyoasisiwa na K.B. Kiingi (1989). Nadharia hii ina sifa maalum ambazo zinasisitiza usasa wa istilahi za lugha, Pia imeweza kujaliza Nadharia ya Istilahi ya Jumla (NIJ) ya Wuester (1931). Ambayo imeeleza kwamba katika uundaji wa istilahi ni lazima muundaji azingatie vigezo fulani vya istilahi zinazofaa, hivyo basi ni Nadharia inayowaongoza wanaistilahi kuunda, kukubali na kukataa istilahi fulani za Kiswahili, hasa zile zisizokuwa na usayansi yaani zile zisizoelezeka kimantiki kwa mujibu wa vigezo tisa vya kisayansi ambavyo hujulikana kama PEGITOSCA ambapo kwa Kiswahili vimefupisha na kuitwa SIZAMASTALIHA yaani usahihi, uiktisadi, uzalishi, umataifa, uangavu, ustaara, utaratibu, ulinganifu na uhalisia. Utafiti huu umefanyika katika taasisi za elimu ya juu zilizoko Zanzibar, vikiwemo Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Chuo Kikuu cha SUMAIT na Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) . Matokeo ya Utafiti yanaonesha kwamba katika maeneo matatu ya kitaaluma yaliyofanyiwa utafiti kiwango cha ukubalifu wa istilahi za TEHAMA za Kiswahili ni kidogo. Sababu kuu ni ugumu na kutoeleweka kimantiki kwa istilahi hizo. Vilevile baadhi ya mbinu za uundaji istilahi zilizotumika zimepelekea kuundwa istilahi ambazo sio rahisi kueleweka. Vilevile mazoea yalioko kwa watumiaji wa TEHAMA ya kutumia lugha chanzi (Kiingereza) pia ni miongoni mwa sababu ya kutokutumika kwa istilahi hizo za Kiswahihili. Aidha kasumba juu ya lugha ya Kiswahili nazo pia ni kikwazo.Kwa mujibu wa utafiti huu istilahi ambazo zimeonekana kukubalika ni zile zilizotafsiriwa au kutoholewa. Pia kuna istilahi ambazo zimezoeleka kutumika zinazotofautiana na zile zilioundwa na mradi (Kilinux). Kwa matokeo haya imebainika kwamba katika jamiilugha ya waswahili walioko Zanzibar hususani wanataaluma, ambao ni watumiaji wakubwa TEHAMA, ni wachache ambao wanakubaliana na istilahi za TEHAMA za Kiswahili zilizoundwa na mradi wa Kilinux. Taarifa hii imeenda sambamba na tathmini nyingine kama vile (Alloni-Feinberg, 1974; Ohly,1979; Mdee, 1980; Mwansoko, 1990; 1993; Sewangi, 1996; Were-Mwaro,2001) zimedhihirisha kuwa baadhi ya Istilahi zilizoundwa rasmi huweza kukataliwa au kutokukubalika na watumiaji wa lugha husika. Licha ya juhudi kubwa ambazo wataalamu wamefanya katika kuisaidia jamii kutumia maarifa haya mapya (TEHAMA) kwa kutumia lugha yao ya Kiswahili, juhudi hizo kwa upande wa Zanzibar zimeonekana kutofanikiwa kama ilivyokusudiwa. Kwa hivyo zoezi la uundaji istilahi lihusishe wanaistilahi na watumiaji wake. Hoja hii imekaziwa nguvu na Mwansoko (1990) kwa kusema, wenye kuhitaji istilahi (watumiaji wa lugha) hawasubiri kuundiwa istilahi na vyombo vya ukuzaji istilahi bali hujiundia istilahi zao wenyewe pale haja inapozuka. Kutokana na hayo, waundaji istilahi wanapaswa kufanya utafiti zaidi juu ya baadhi ya istilahi nyingine ambazo hazijafanyiwa utafiti, ili waweze kuwasaidia watumiaji wa mtandao kwa lugha ya Kiswahili kwa kuunda istilahi rahisi ambazo zitakuwa ni rahisi kueleweka, kukubalika na kutumika vizuri.
- ItemKuchunguza Motifu za Kisasi katika Hadithi Simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja(2019-04) KUTUTWA, Ramadhan AbdalaUtafiti huu ulilenga kuchunguza motifu za visasi katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Motifu ni miegamo ambayo fanani wa kazi za fasihi huiegemea katika kuzijenga kazi zao. Visasi ni aina ya hukumu, ambayo mara nyingi, huchukuliwa na kutekelezwa pale pasipokuwa na maadili ya kikanuni. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni; kubainisha aina za motifu za kisasi zinavyojitokeza katika hadithi simulizi, kubainisha sababu za kulipizana kisasi katika hadithi simulizi, na lengo la tatu ni kuchunguza uhalisia wa visasi kwenye jamii ya mkoa wa Mjini Magharibi. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kuchambua motifu za visasi zinazojitokeza katika hadithi simulizi na uhalisia wa visasi katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni maktaba na uwandani. Data zilizokusanywa zimechambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha uhalisia wa visasi ndani ya jamii ya watu wa Mkoa wa Mjini Magharibi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, kuna aina tatu za motifu za visasi ambazo ni motifu za visasi vya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa upande wa sababu za visasi, matokeo ya utafiti yamebaini kuwa kuna sababu kama vile chuki ya mali, dhuluma, wivu, bezo na husda. Aidha lengo la mwisho la utafiti huu, limebaini uhalisia wa visasi vinavyotokana na uchumi na jamii. Utafiti huu ni muhimu kwani umesaidia kuchunguza na kubainisha motifu za kisasi zilizomo katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibui Unguja na hivyo utawasaidia wengi miongoni mwa wasomi na wanajamii kwa ujumla.
- ItemMAANA FICHE YA MANENO YANAYOTUMIWA NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA ZANZIBAR(SUZA, 2021-12-01) RAMADHAN, Saada JumaUtafiti huu umechunguza “Maana Fiche ya Maneno Yanayotumiwa na Waathirika wa Dawa za Kulevya Zanzibar”. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni; Kubainisha maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kufafanua maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kujadili sababu za matumizi ya maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar pamoja na kutathmini athari za maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar. Nadharia ya Maana ni Matumizi iliyoasisiwa na Wittgenstein (1933) na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano ya Giles (1973) zimetumika kuuongoza utafiti huu. Jumla ya watoa taarifa 73 walishirikishwa katika utafiti huu. Data zimekusanywa kwa mbinu ya usaili, mjadala wa kundi lengwa na ushuhudiaji. Uchambuzi wa data umefanywa kwa njia ya maelezo na majadweli yametumika pale ilipohitajika. Jumla ya maneno mia moja na sita (106) yenye maana fiche yamekusanywa na kuchambuliwa. Maana fiche za maneno zimechambuliwa kwa kuzingatia; aina ya dawa za kulevya, Vipimo vya dawa za kulevya na maana fiche zinazohusu taasisi zinazopambana na dawa za kulevya. Vilevile, sababu tano za matumizi ya maana fiche zimebainika; sababu za kiusalama, kutunza siri, kuwatia hofu wanajamii, kuogopa unyanyapaa wa wanajamii na kujitofautisha na wanajamii wengine. Athari sita za matumizi ya maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar zimejitokeza. Athari hizo ni; kuharibu lugha ya Kiswahili, mwendelezo wa uingizwaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya, kuathiri harakati za mapambano dhidi ya dawa hizo, ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya, kuathiri mawasiliano baina ya wahudumu na waathirika wa dawa za kulevya na kuipotosha jamii. Kwa kuwa utafiti huu umechunguza lugha ya waathirika wa dawa za kulevya katika uga wa semantiki, mtafiti amependekeza tafiti zijazo ziangazie katika nyanja nyingine kama vile fonolojia, mofolojia na sintaksi
- ItemMAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI(SUZA, 2022-12-01) jAKU,Mwanaidi JumaUtafiti huu ulichunguza makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni na kueleza sababu za makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulifanyika Zanzibar, data zilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na kituo cha Kiswahili na Utamaduni kwa walimu na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika vituo hivyo. Mbinu za uchambuzi wa nyaraka na usaili ndizo zilizotumika kukusanyia data hizo na uchambuzi wa data hizo ulitumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa (UM) iliyoasisiwa na Corder (1967), makosa mbalimbali yaligunduliwa katika utafiti huu yakiwemo makosa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya mnyambuliko wa hali za vitenzi, matumizi ya msamiati usiofaa katika muktadha wake, kutenganisha maneno pasipostahiki, udondoshaji wa kitamkwa katika neno, makosa ya tafsiri sisisi, udondoshaji wa maneno katika sentensi, kuunganisha maneno mahali pasipostahiki na kubadili mpangilio wa fonimu. Utafiti huu pia ulibaini sababu za makosa hayo ambazo ni pamoja na athari ya lugha ya kwanza ya mwanafunzi, ugumu wa sheria za lugha ya pili na sababu nyengine ni ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wanafunzi. Aidha, utafiti huu umetoa mapendekezo kwa walimu, wanafunzi pamoja na tafiti zijazo
- ItemMatumizi ya Kipashio "ni" katika Kitumbatu(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-11) HIJA, Silima HajiUtafiti huu unahusu matumizi ya kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Utafiti umefanywa katika Wilaya ya Kaskazini A, katika Wilaya ndogo ya Tumbatu, Unguja, Zanzibar. Data za msingi zimepatikana kwa njia ya usaili, uchunguzi makini na masimulizi kutoka kwa wanafunzi na walimu wa Skuli za Sekondari za Tumbatu pamoja na wazee kutoka katika shehia ya Jongowe na Gomani. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha aina za maneno ambazo huchukua kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu. Kufafanua mazingira ya utokeaji wa kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Kujadili dhima ya kipashio ‘ni’ katika maneno ya Kitumbatu. Nadharia ya Umuundo imetumika katika utafiti huu. Utafiti umeonesha kuwa kipashio ‘ni’ katika Kitumbatu kina matumizi mbalimbali kwa watumiaji wa lahaja hiyo yaani Watumbatu. Miongoni mwa matumizi hayo ni kipashio ‘ni’ kama kiwakilishi cha nafsi ya kwanza umoja mtenda na mtendwa, kielezi cha mahali, kiwakilisha cha tukio, mzizi wa neno wenye hadhi ya swali na kitenzi kishirikishi. Utafiti huu ni muhuimu kwa sababu unawasaidia walimu, wanafunzi na watafiti wa somo la lughawiya katika kupata marejeo.
- ItemMATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA(SUZA, 2022-12-01) ALI,Maryam KomboUtafiti huu unahusu matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi „B‟ Kisiwani Unguja na kuhusisha kampuni ya Progressive Marketing Company Limited na Sumbezi Marketing Directing. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Jumla ya watoataarifa 29 walihusishwa katika utafiti huu. Mazungumzo kumi (10) ya kimaandishi yalichanganuliwa ili kupata data ya mikakati ya upole kukidhi lengo la kwanza. Data hiyo ilipatikana kupitia mbinu ya ushuhudiaji, hata hivyo mbinu ya mahojiano ilitumika kupata maoni yaliyolikamilisha lengo la pili. Hatimaye uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo.Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987). Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wauza bidhaa za promosheni majumbani hutumia mikakati minne ya upole yaani; mkakati wa kuzungumza kwa uwazi, mkakati wa upole chanya, mkakati wa upole hasi na mkakati wa kuzungumza kwa kuficha katika mazungumzo yao wakati wanapoamiliana na wateja wao. Halikadhalika kupitia data ya maoni, wasailiwa walikiri kuwa matumizi ya lugha ya upole husaidia kujenga heshima, kukuza mahusiano mazuri baina ya wauzaji na wanunuzi na kuongeza mauzo katika biashara yao. Kwa ujumla, utafiti unapendekeza kufanyika kwa tafiti zaidi zitakazobainisha vipengele vya kilughawiya vinavyounda lugha ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.
- ItemMatumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili(SUZA, 2018-01-01) HAJI USSI, NADHRAUtafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika kukusanya data za maktabani, mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia makala mbalimbali zinazohusiana na utafit huu. Kwa upande wa data za uwandani, mtafiti alitumia mbinu ya usaili, hojaji na uchunguzi makinifu kwa kutumia usampulishaji mdokezo na lengwa. Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia mkabala wa kiidadi na mkabala stahilifu. Hata hivyo, mikabala yote ilitumika pale palipohitajika. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ilitumika kuchambulia data zinazohusiana malengo mahsusi ya utafiti huu na Nadharia ya Maana ni Matumizi ilitumika kuchambua data kwa pale panapostahiki. Matokeo ya utafiti huu, yaliweza kutupatia sifa tafauti za kiuzungumzaji katika maneno na mitindo ya sentensi katika kipengele cha sauti, maneno, sentensi na maana. Pia utokeaji wa lugha ya Kiswahili katika miktadha mbalimbali unatafautiana kimaana na kimuundo na unafafana katika utumiaji wa baadhi maneno na kwa upande wa kiisimu tuliweza kubaini changamoto hasi katika fonolojia, mofolojia, sintaksia na msamiati na chanya katika semantiki na msamiati, aidha kwa upande usio wa kiisimu tuliweza kupata changamoto hasi zaidi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mtafiti anapendekeza kuwa jamii itoe taaluma maalumu itakayoshughulikia kuthibiti na kuhifadhi matumizi sahihi ya lugha.
- ItemMatumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari zake kwa Watoto Zanzibar(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) HAFIDH, Zainab AliUtafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto. Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahili
- ItemMATUMIZI YA LUGHA YA WAZEE WA KIKE NA ATHARI ZAKE KWA WATOTO ZANZIBAR(SUZA, 2018-01-20) HAFIDH, Zainab AliUtafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto.Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahil
- ItemMATUMIZI YA TASWIRA KATIKA KUJENGA DHAMIRA ZA NGANO ZA HURAFA: VITONGOJI PEMBA(SUZA, 2020-08-19) MBAROUK, Asha AliUtafiti huu umechunguza Matumizi ya Taswira Katika Kujenga Dhamira za Ngano za Hurafa, Vitongoji Pemba. Tatizo la utafiti lilikuwa ni kutokuchunguzwa na wataalamu matumizi ya taswira katika ngano za hurafa, Vitongoji Pemba. Kwa sababu katika mapitio yaliyodurusiwa haikuonekana kazi yoyote ya utafiti ambayo imeichunguza mada hiyo. Matokeo ya utafiti huu yameweza kubainisha taswira mbalimbali zinazopatikana katika ngano za hurafa na kuonesha jinsi zinavyojenga dhamira. Utafiti umekuwa na malengo matatu; Kubainisha aina za taswira zinazopatikana katika ngano za hurafa, kuchunguza dhamira jinsi zinavyojengwa na taswira, na mwisho, ni kuhusisha dhamira za taswira na maisha ya jamii ya Pemba. Mtafiti ametumia data za uwandani kwa kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, walimu na wanafunzi. Data za msingi zimekuwa ni ngano zilizokusanywa kutoka kwa wazee, pamoja na maoni ya watoa taarifa yaliyokusanywa kupitia majadiliano ya vikundi, usaili na usomaji maktaba. Utafiti umeongozwa na nadharia mbili. Nadharia ya Uamilifu iliyotumika kuangalia aina za taswira na dhamira zinazoibuka. Nadharia nyingine ilikuwa Nadharia ya Semiotiki ambayo imetumika kufafanua maana za ishara na kuzihusisha na maisha ya jamii ya Pemba. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa ngano zinazo taswira zinazoibua dhamira mbali mbali na kuwa na uhusiano wa moja kwa moja, na ndiyo maana kizazi hadi kizazi cha Pemba hurithishwa nazo
- «
- 1 (current)
- 2
- 3
- »