Kuchunguza Motifu za Kisasi katika Hadithi Simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja

No Thumbnail Available
Date
2019-04
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza motifu za visasi katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Motifu ni miegamo ambayo fanani wa kazi za fasihi huiegemea katika kuzijenga kazi zao. Visasi ni aina ya hukumu, ambayo mara nyingi, huchukuliwa na kutekelezwa pale pasipokuwa na maadili ya kikanuni. Malengo mahususi ya utafiti huu yalikuwa ni; kubainisha aina za motifu za kisasi zinavyojitokeza katika hadithi simulizi, kubainisha sababu za kulipizana kisasi katika hadithi simulizi, na lengo la tatu ni kuchunguza uhalisia wa visasi kwenye jamii ya mkoa wa Mjini Magharibi. Nadharia ya Uhalisia ilitumika kuchambua motifu za visasi zinazojitokeza katika hadithi simulizi na uhalisia wa visasi katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni maktaba na uwandani. Data zilizokusanywa zimechambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha uhalisia wa visasi ndani ya jamii ya watu wa Mkoa wa Mjini Magharibi. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba, kuna aina tatu za motifu za visasi ambazo ni motifu za visasi vya kisiasa, kiuchumi na kijamii. Kwa upande wa sababu za visasi, matokeo ya utafiti yamebaini kuwa kuna sababu kama vile chuki ya mali, dhuluma, wivu, bezo na husda. Aidha lengo la mwisho la utafiti huu, limebaini uhalisia wa visasi vinavyotokana na uchumi na jamii. Utafiti huu ni muhimu kwani umesaidia kuchunguza na kubainisha motifu za kisasi zilizomo katika hadithi simulizi za Mkoa wa Mjini Magharibui Unguja na hivyo utawasaidia wengi miongoni mwa wasomi na wanajamii kwa ujumla.
Description
Available in print form at Tunguu Lending Library
Keywords
1. Aina za motifu za kisasi zinavyojitokeza katika hadithi simulizi, 2. Sababu za kulipizana kisasi katika hadithi simulizi, 3. Uhalisia wa visasi kwenye jamii ya mkoa wa Mjini Magharibi.
Citation
Ramadal Abdala Kututwa