MAANA FICHE YA MANENO YANAYOTUMIWA NA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA ZANZIBAR

No Thumbnail Available
Date
2021-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu umechunguza “Maana Fiche ya Maneno Yanayotumiwa na Waathirika wa Dawa za Kulevya Zanzibar”. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni; Kubainisha maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kufafanua maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kujadili sababu za matumizi ya maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar pamoja na kutathmini athari za maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar. Nadharia ya Maana ni Matumizi iliyoasisiwa na Wittgenstein (1933) na Nadharia Kidhi ya Mawasiliano ya Giles (1973) zimetumika kuuongoza utafiti huu. Jumla ya watoa taarifa 73 walishirikishwa katika utafiti huu. Data zimekusanywa kwa mbinu ya usaili, mjadala wa kundi lengwa na ushuhudiaji. Uchambuzi wa data umefanywa kwa njia ya maelezo na majadweli yametumika pale ilipohitajika. Jumla ya maneno mia moja na sita (106) yenye maana fiche yamekusanywa na kuchambuliwa. Maana fiche za maneno zimechambuliwa kwa kuzingatia; aina ya dawa za kulevya, Vipimo vya dawa za kulevya na maana fiche zinazohusu taasisi zinazopambana na dawa za kulevya. Vilevile, sababu tano za matumizi ya maana fiche zimebainika; sababu za kiusalama, kutunza siri, kuwatia hofu wanajamii, kuogopa unyanyapaa wa wanajamii na kujitofautisha na wanajamii wengine. Athari sita za matumizi ya maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar zimejitokeza. Athari hizo ni; kuharibu lugha ya Kiswahili, mwendelezo wa uingizwaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya, kuathiri harakati za mapambano dhidi ya dawa hizo, ongezeko la watumiaji wa dawa za kulevya, kuathiri mawasiliano baina ya wahudumu na waathirika wa dawa za kulevya na kuipotosha jamii. Kwa kuwa utafiti huu umechunguza lugha ya waathirika wa dawa za kulevya katika uga wa semantiki, mtafiti amependekeza tafiti zijazo ziangazie katika nyanja nyingine kama vile fonolojia, mofolojia na sintaksi
Description
Utafiti huu umechunguza “Maana Fiche ya Maneno Yanayotumiwa na Waathirika wa Dawa za Kulevya Zanzibar”. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni; Kubainisha maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kufafanua maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar, kujadili sababu za matumizi ya maana fiche ya maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar pamoja na kutathmini athari za maana fiche za maneno yanayotumiwa na waathirika wa dawa za kulevya Zanzibar
Keywords
Citation