Matumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili
No Thumbnail Available
Date
2018-01-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na
Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza
matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika
Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika
kukusanya data za maktabani, mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa lugha ya
Kiswahili kupitia makala mbalimbali zinazohusiana na utafit huu. Kwa upande wa data za
uwandani, mtafiti alitumia mbinu ya usaili, hojaji na uchunguzi makinifu kwa kutumia
usampulishaji mdokezo na lengwa. Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia
mkabala wa kiidadi na mkabala stahilifu. Hata hivyo, mikabala yote ilitumika pale
palipohitajika. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ilitumika kuchambulia data
zinazohusiana malengo mahsusi ya utafiti huu na Nadharia ya Maana ni Matumizi
ilitumika kuchambua data kwa pale panapostahiki. Matokeo ya utafiti huu, yaliweza
kutupatia sifa tafauti za kiuzungumzaji katika maneno na mitindo ya sentensi katika
kipengele cha sauti, maneno, sentensi na maana. Pia utokeaji wa lugha ya Kiswahili katika
miktadha mbalimbali unatafautiana kimaana na kimuundo na unafafana katika utumiaji wa
baadhi maneno na kwa upande wa kiisimu tuliweza kubaini changamoto hasi katika
fonolojia, mofolojia, sintaksia na msamiati na chanya katika semantiki na msamiati, aidha
kwa upande usio wa kiisimu tuliweza kupata changamoto hasi zaidi. Kutokana na matokeo
ya utafiti huu, mtafiti anapendekeza kuwa jamii itoe taaluma maalumu itakayoshughulikia
kuthibiti na kuhifadhi matumizi sahihi ya lugha.
Description
Utafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na
Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza
matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika
Kiswahili.
Keywords
1. Matumizi ya Lugha ya Vijana - Kiswahili 2. Lugha - Kiswahili 3. Changamoto za lugha - Vijana wa Kizanzibar