Matumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili

dc.contributor.authorHAJI USSI, NADHRA
dc.date.accessioned2020-08-22T19:50:09Z
dc.date.available2020-08-22T19:50:09Z
dc.date.issued2018-01-01
dc.descriptionUtafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili.en_US
dc.description.abstractUtafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili. Data za utafiti huu zilikusanywa kutoka maktabani na uwandani. Katika kukusanya data za maktabani, mtafiti alifanya uchunguzi na uchambuzi wa lugha ya Kiswahili kupitia makala mbalimbali zinazohusiana na utafit huu. Kwa upande wa data za uwandani, mtafiti alitumia mbinu ya usaili, hojaji na uchunguzi makinifu kwa kutumia usampulishaji mdokezo na lengwa. Katika kuzichambua data hizo, mtafiti alitumia mkabala wa kiidadi na mkabala stahilifu. Hata hivyo, mikabala yote ilitumika pale palipohitajika. Nadharia ya Uchunguzi wa Kimaeneo ilitumika kuchambulia data zinazohusiana malengo mahsusi ya utafiti huu na Nadharia ya Maana ni Matumizi ilitumika kuchambua data kwa pale panapostahiki. Matokeo ya utafiti huu, yaliweza kutupatia sifa tafauti za kiuzungumzaji katika maneno na mitindo ya sentensi katika kipengele cha sauti, maneno, sentensi na maana. Pia utokeaji wa lugha ya Kiswahili katika miktadha mbalimbali unatafautiana kimaana na kimuundo na unafafana katika utumiaji wa baadhi maneno na kwa upande wa kiisimu tuliweza kubaini changamoto hasi katika fonolojia, mofolojia, sintaksia na msamiati na chanya katika semantiki na msamiati, aidha kwa upande usio wa kiisimu tuliweza kupata changamoto hasi zaidi. Kutokana na matokeo ya utafiti huu, mtafiti anapendekeza kuwa jamii itoe taaluma maalumu itakayoshughulikia kuthibiti na kuhifadhi matumizi sahihi ya lugha.en_US
dc.description.sponsorshipSUZAen_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/171
dc.language.isootheren_US
dc.publisherSUZAen_US
dc.subject1. Matumizi ya Lugha ya Vijana - Kiswahili 2. Lugha - Kiswahili 3. Changamoto za lugha - Vijana wa Kizanzibaren_US
dc.titleMatumizi ya Lugha ya Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahilien_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
Nadhra PDF.pdf
Size:
380.85 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Utafiti huu, ulijihusisha na Matumizi ya Lugha ya Kiswahili kwa Vijana wa Kizanzibar na Changamoto zake katika Kiswahili. Mtafiti alitumia mbinu mbalimbali katika kuchunguza matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vijana wa Kizanzibari na changamoto zake katika Kiswahili.
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: