Dhima za Majina katika Nyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Kitumbatu

No Thumbnail Available
Date
2018-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu ulifanywa kwa nia kuu ya kuchunguza “Dhima za Majina katika Vyombo vya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Malengo mahsusi ya ufafiti huu yalikuwa kuchambua maana ya majina katika vyombo vya uvuvi, kuchunguza dhima za majina ya vyombo hivyp katika jamii husika, na kubainisha athari za majina ya vyombovya uvuvi kwa jamii yaTumbatu. Ili kufanikisha utafiti huu,nadharia ya Upokeaji na Semiotiki zilitumika, Mbinu za kukusanya data zilizotumika katika utafiti huu ni pamoja na maktaba na mahojiano ya ana kwa ana. Data zilizokusanywa zilichambuliwa kwa kutolewa ufafanuzi wa kimaelezo na mjadala. Matokeo ya uchanganuzi wa data yaliweza kujibu maswali ya utafiti, kwani yalibainisha “Dhima za Majina katika Vyombovya Uvuvi kwa Jamii ya Tumbatu”.Mtokeo ya utafiti huu yameonesha kuwa, majina yamegawika katika makundi tofauti na kunasibishwa katika makundi hayo kulingana na maana yake kifasihi. Makundi hayo ni majazi, misimu, mafumbo jina, lakabu na mafumbo ya kiimani. Kwa upande wa dhima za majina hayo nipamoja nakutunza historia na matukio muhimu ya jamii, kutambulisha chombo katika taasisi rasmi, kudokeza wasifu wa chombo, nahodha na hata mmiliki wa chombo.Majina hayo yanaendeleza majina na kueleza fasihi pamoja na kujenga utani katika jamii. Na kwa upande wa athari; athari chanya ni kutumika katika usajili, kutofautisha chombo kimoja na kingine, kuendeleza vipawa vya wanajamii, kutumika kama ni dafina ya kuhifadhia matukio ya kijamii na mambo ya kihostoria. Na, athari hasi; majinahutumika kuendeleza chuki na uhasama baina ya wanajamii na kujenga mazingira ya hasada na mikosi juu ya chombo pamoja na kubomoa na kuchafuamaadili ya jamii husika.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Majina katika vyombo vya uvuvi Tumbatu - Dhima 2. Majina katika vyombo vya uvuvi Tumbatu - Maana 3. Majina katika vyombo vya uvuvi Tumbatu - Athari
Citation