Dhima za Taharuki katika Riwaya za Kiswahili: Kisima cha Giningi ma Mzimu wa Watu wa Kale

No Thumbnail Available
Date
2019-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu umechunguza dhima za taharuki katika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale na Kisima cha Giningi zilizotungwa na Muhammed Said Abdulla. Utafiti huu umefanyika katika mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Data zake za msingi zimepatikana kwa njia ya maktaba, usaili kwa walimu na mahojiano kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Njia ya maktaba ilimuwezesha mtafiti kusoma riwaya zilizoteuliwa na kupata data za msingi ambazo zilitumika katika uchanganuzi. Data nyingine zilizopatikana kwa njia ya usaili na mahojiano zimetumika kutilia mkazo na kuzihakikisha data zilizopatikana kwa njia ya maktaba katika kufikiwa malengo ya utafiti. Malengo hayo ni kuainisha aina za taharuki, kufafanua mazingira ya utokeaji wake na kuelezea dhima zake. Matokeo ya utafiti yamebainisha aina za taharuki, mazingira yake na dhima zake, kwa kuongozwa na Nadharia ya Umuundo na Nadharia ya Uamilifu. Nadharia ya Umuundo imesaidia kuangalia aina za taharuki; taharuki msingi, taharuki ndogo na taharuki hamasishi na mazingira yake. Nadharia ya Uamilifu imetumika kuangalia dhima zake. Utafiti umeonesha kuwa ipo haja ya kuchunguzwa tena kipengele hiki cha taharuki katika tanzu nyingine za fasihi ya Kiswahili.
Description

Keywords
DHIMA ZA TAHARUKI KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI: Kisima cha Giningi na Mzimu wa Watu wa Kale
Citation