MAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI

No Thumbnail Available
Date
2022-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulichunguza makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni na kueleza sababu za makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulifanyika Zanzibar, data zilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na kituo cha Kiswahili na Utamaduni kwa walimu na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika vituo hivyo. Mbinu za uchambuzi wa nyaraka na usaili ndizo zilizotumika kukusanyia data hizo na uchambuzi wa data hizo ulitumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa (UM) iliyoasisiwa na Corder (1967), makosa mbalimbali yaligunduliwa katika utafiti huu yakiwemo makosa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya mnyambuliko wa hali za vitenzi, matumizi ya msamiati usiofaa katika muktadha wake, kutenganisha maneno pasipostahiki, udondoshaji wa kitamkwa katika neno, makosa ya tafsiri sisisi, udondoshaji wa maneno katika sentensi, kuunganisha maneno mahali pasipostahiki na kubadili mpangilio wa fonimu. Utafiti huu pia ulibaini sababu za makosa hayo ambazo ni pamoja na athari ya lugha ya kwanza ya mwanafunzi, ugumu wa sheria za lugha ya pili na sababu nyengine ni ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wanafunzi. Aidha, utafiti huu umetoa mapendekezo kwa walimu, wanafunzi pamoja na tafiti zijazo
Description
Mbinu za uchambuzi wa nyaraka na usaili ndizo zilizotumika kukusanyia data hizo na uchambuzi wa data hizo ulitumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa (UM) iliyoasisiwa na Corder (1967), makosa mbalimbali yaligunduliwa katika utafiti huu yakiwemo makosa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya mnyambuliko wa hali za vitenzi, matumizi ya msamiati usiofaa katika muktadha wake,
Keywords
Citation