MAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI

dc.contributor.authorjAKU,Mwanaidi Juma
dc.date.accessioned2024-04-24T08:28:27Z
dc.date.available2024-04-24T08:28:27Z
dc.date.issued2022-12-01
dc.descriptionMbinu za uchambuzi wa nyaraka na usaili ndizo zilizotumika kukusanyia data hizo na uchambuzi wa data hizo ulitumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa (UM) iliyoasisiwa na Corder (1967), makosa mbalimbali yaligunduliwa katika utafiti huu yakiwemo makosa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya mnyambuliko wa hali za vitenzi, matumizi ya msamiati usiofaa katika muktadha wake,
dc.description.abstractUtafiti huu ulichunguza makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulikuwa na malengo mawili ambayo ni kubainisha makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni na kueleza sababu za makosa ya kisemantiki yanayofanywa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulifanyika Zanzibar, data zilikusanywa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na kituo cha Kiswahili na Utamaduni kwa walimu na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika vituo hivyo. Mbinu za uchambuzi wa nyaraka na usaili ndizo zilizotumika kukusanyia data hizo na uchambuzi wa data hizo ulitumia mkabala wa kimaelezo. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Uchanganuzi wa Makosa (UM) iliyoasisiwa na Corder (1967), makosa mbalimbali yaligunduliwa katika utafiti huu yakiwemo makosa yanayosababishwa na matumizi mabaya ya mnyambuliko wa hali za vitenzi, matumizi ya msamiati usiofaa katika muktadha wake, kutenganisha maneno pasipostahiki, udondoshaji wa kitamkwa katika neno, makosa ya tafsiri sisisi, udondoshaji wa maneno katika sentensi, kuunganisha maneno mahali pasipostahiki na kubadili mpangilio wa fonimu. Utafiti huu pia ulibaini sababu za makosa hayo ambazo ni pamoja na athari ya lugha ya kwanza ya mwanafunzi, ugumu wa sheria za lugha ya pili na sababu nyengine ni ukosefu wa mazoezi miongoni mwa wanafunzi. Aidha, utafiti huu umetoa mapendekezo kwa walimu, wanafunzi pamoja na tafiti zijazo
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherMETK/3/19/013/TZ SUZA
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/259
dc.language.isoother
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries00001; 2022
dc.titleMAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MAKOSA YA KISEMANTIKI YANAYOFANYWA NA WANAFUNZI WANAOJIFUNZA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI.pdf
Size:
1.7 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: