MATUMIZI YA LUGHA YA WAZEE WA KIKE NA ATHARI ZAKE KWA WATOTO ZANZIBAR

Loading...
Thumbnail Image
Date
2018-01-20
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto.Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahil
Description
Utafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”
Keywords
Citation