MATUMIZI YA TASWIRA KATIKA KUJENGA DHAMIRA ZA NGANO ZA HURAFA: VITONGOJI PEMBA

No Thumbnail Available
Date
2020-08-19
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu umechunguza Matumizi ya Taswira Katika Kujenga Dhamira za Ngano za Hurafa, Vitongoji Pemba. Tatizo la utafiti lilikuwa ni kutokuchunguzwa na wataalamu matumizi ya taswira katika ngano za hurafa, Vitongoji Pemba. Kwa sababu katika mapitio yaliyodurusiwa haikuonekana kazi yoyote ya utafiti ambayo imeichunguza mada hiyo. Matokeo ya utafiti huu yameweza kubainisha taswira mbalimbali zinazopatikana katika ngano za hurafa na kuonesha jinsi zinavyojenga dhamira. Utafiti umekuwa na malengo matatu; Kubainisha aina za taswira zinazopatikana katika ngano za hurafa, kuchunguza dhamira jinsi zinavyojengwa na taswira, na mwisho, ni kuhusisha dhamira za taswira na maisha ya jamii ya Pemba. Mtafiti ametumia data za uwandani kwa kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, walimu na wanafunzi. Data za msingi zimekuwa ni ngano zilizokusanywa kutoka kwa wazee, pamoja na maoni ya watoa taarifa yaliyokusanywa kupitia majadiliano ya vikundi, usaili na usomaji maktaba. Utafiti umeongozwa na nadharia mbili. Nadharia ya Uamilifu iliyotumika kuangalia aina za taswira na dhamira zinazoibuka. Nadharia nyingine ilikuwa Nadharia ya Semiotiki ambayo imetumika kufafanua maana za ishara na kuzihusisha na maisha ya jamii ya Pemba. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa ngano zinazo taswira zinazoibua dhamira mbali mbali na kuwa na uhusiano wa moja kwa moja, na ndiyo maana kizazi hadi kizazi cha Pemba hurithishwa nazo
Description
Utafiti huu umechunguza Matumizi ya Taswira Katika Kujenga Dhamira za Ngano za Hurafa, Vitongoji Pemba.
Keywords
Citation