MATUMIZI YA TASWIRA KATIKA KUJENGA DHAMIRA ZA NGANO ZA HURAFA: VITONGOJI PEMBA

dc.contributor.authorMBAROUK, Asha Ali
dc.date.accessioned2024-04-18T07:28:20Z
dc.date.available2024-04-18T07:28:20Z
dc.date.issued2020-08-19
dc.descriptionUtafiti huu umechunguza Matumizi ya Taswira Katika Kujenga Dhamira za Ngano za Hurafa, Vitongoji Pemba.
dc.description.abstractUtafiti huu umechunguza Matumizi ya Taswira Katika Kujenga Dhamira za Ngano za Hurafa, Vitongoji Pemba. Tatizo la utafiti lilikuwa ni kutokuchunguzwa na wataalamu matumizi ya taswira katika ngano za hurafa, Vitongoji Pemba. Kwa sababu katika mapitio yaliyodurusiwa haikuonekana kazi yoyote ya utafiti ambayo imeichunguza mada hiyo. Matokeo ya utafiti huu yameweza kubainisha taswira mbalimbali zinazopatikana katika ngano za hurafa na kuonesha jinsi zinavyojenga dhamira. Utafiti umekuwa na malengo matatu; Kubainisha aina za taswira zinazopatikana katika ngano za hurafa, kuchunguza dhamira jinsi zinavyojengwa na taswira, na mwisho, ni kuhusisha dhamira za taswira na maisha ya jamii ya Pemba. Mtafiti ametumia data za uwandani kwa kutumia sampuli lengwa. Walengwa wa utafiti huu ni wazee, walimu na wanafunzi. Data za msingi zimekuwa ni ngano zilizokusanywa kutoka kwa wazee, pamoja na maoni ya watoa taarifa yaliyokusanywa kupitia majadiliano ya vikundi, usaili na usomaji maktaba. Utafiti umeongozwa na nadharia mbili. Nadharia ya Uamilifu iliyotumika kuangalia aina za taswira na dhamira zinazoibuka. Nadharia nyingine ilikuwa Nadharia ya Semiotiki ambayo imetumika kufafanua maana za ishara na kuzihusisha na maisha ya jamii ya Pemba. Matokeo ya utafiti yamebainisha kuwa ngano zinazo taswira zinazoibua dhamira mbali mbali na kuwa na uhusiano wa moja kwa moja, na ndiyo maana kizazi hadi kizazi cha Pemba hurithishwa nazo
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherTHESIS
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/242
dc.language.isoen
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries2020
dc.titleMATUMIZI YA TASWIRA KATIKA KUJENGA DHAMIRA ZA NGANO ZA HURAFA: VITONGOJI PEMBA
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MATUMIZI YA TASWIRA KATIKA KUJENGA DHAMIRA ZA NGANO ZA HURAFA: VITONGOJI PEMBA.pdf
Size:
374.64 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: