Uundaji wa Istilahi za Kiswaili: Mfano wa Istilahi za Sayansi ya Kumpyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

No Thumbnail Available
Date
2018-10-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kupitia orodha za istilahi za uwanja huo pamoja na ujazaji wa dodoso na mahojiano ya kundi lengwa ambalo lilihusisha wataalamu na wanafunzi wa taaluma hizo. Imegundulika kwamba takriban asilimia 50 tu ya istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA zinazofahamika kwa watumiaji wake. Aidha, istilahi zinazokubalika kwa watumiaji ni asilimia 51. Hivyo, kuna uhusiano mkubwa kati ya kufahamika kwa istilahi na kukubalika kwake. Utafiti pia umegundua kwamba sababu zilizochangia kutokubalika kwa baadhi ya istilahi ni pamoja na maana ya istilahi hizo kuwa tafauti na maana ya asili katika Kiingereza, ugumu wa kufahamika kwa istilahi, kwenda kinyume na utamaduni wa Waswahili na kutopendwa na watumiaji. Kwa upande wa Mlango wa Lugha, imebainika kwamba baadhi ya istilahi zinakwenda kinyume na kanuni za kisarufi za miundo ya maneno ya Kiswahili, ikiwemo miundo ya silabi na maneno isiyokubalika kwa mujibu wa kanuni za Kiswahili.
Description
Utafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu
Keywords
1. Istilahi za Kiswahili 2. Istilahi za Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - Kiswahili
Citation