Uundaji wa Istilahi za Kiswaili: Mfano wa Istilahi za Sayansi ya Kumpyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

dc.contributor.authorSALEH KHALFAN, ALLY
dc.date.accessioned2020-08-22T19:37:14Z
dc.date.available2020-08-22T19:37:14Z
dc.date.issued2018-10-01
dc.descriptionUtafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huuen_US
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu. Data za utafiti zilikusanywa kwa kupitia orodha za istilahi za uwanja huo pamoja na ujazaji wa dodoso na mahojiano ya kundi lengwa ambalo lilihusisha wataalamu na wanafunzi wa taaluma hizo. Imegundulika kwamba takriban asilimia 50 tu ya istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA zinazofahamika kwa watumiaji wake. Aidha, istilahi zinazokubalika kwa watumiaji ni asilimia 51. Hivyo, kuna uhusiano mkubwa kati ya kufahamika kwa istilahi na kukubalika kwake. Utafiti pia umegundua kwamba sababu zilizochangia kutokubalika kwa baadhi ya istilahi ni pamoja na maana ya istilahi hizo kuwa tafauti na maana ya asili katika Kiingereza, ugumu wa kufahamika kwa istilahi, kwenda kinyume na utamaduni wa Waswahili na kutopendwa na watumiaji. Kwa upande wa Mlango wa Lugha, imebainika kwamba baadhi ya istilahi zinakwenda kinyume na kanuni za kisarufi za miundo ya maneno ya Kiswahili, ikiwemo miundo ya silabi na maneno isiyokubalika kwa mujibu wa kanuni za Kiswahili.en_US
dc.description.sponsorshipSUZAen_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/169
dc.language.isoenen_US
dc.publisherSUZAen_US
dc.subject1. Istilahi za Kiswahili 2. Istilahi za Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano - Kiswahilien_US
dc.titleUundaji wa Istilahi za Kiswaili: Mfano wa Istilahi za Sayansi ya Kumpyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasilianoen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
TASNIFU YA UZAMIVU -ALLY SALEH KHALFAN.pdf
Size:
3.54 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Utafiti huu ulilenga kuchunguza ufanisi katika uundaji wa istilahi za Kiswahili. Ufanisi huu uliangaliwa katika maeneo makuu matatu; namna istilahi zinavyofuata kaida za kisarufi za Kiswahili, kufahamika istilahi hizo kwa watumiaji wake na kukubalika kwake. Utafiti ulijikita katika istilahi za Sayansi ya Kompyuta na TEHAMA. Nadharia ya Milango (Theory of Doors) iliyoasisiwa na Cabré (2003) ndiyo iliyotumika kuongoza utafiti huu
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: