Sanaa na Mshikamano wa Maudhui katika Vitendawili

No Thumbnail Available
Date
2018-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu umechunguza mshikamano uliopo katika sanaa ya vitendawili na maudhui ya vitendawili hivyo. Utafiti umeangalia vipengele vya kisanaa kadhaa kama vile; sauti, mapigo ya kimuziki yatokanayo na urari wa vina na mizani, lugha ya picha na ishara, tamathali za semi na kadhalika. Pia umechambua maandiko mengi yaliyohusu uchambuzi wa kimaudhui wa vitendawili mbalimbali vya ndani na nje ya jamii hii. Uchambuzi huo umesaidia kuviainisha vipengele tafauti vya kimaudhui vinavyojitokeza katika utanzu huu. Dhamira kadhaa zinazosadifu jamii ya Zanzibar zilionekana ingawa ni kwa ufupi mno. Kutokana na uchambuzi wa kifani na kimaudhui uliojadiliwa, mtafiti amepata nafasi ya kuchambua mshikamano unaojitokeza kupitia sanaaa ya vitendawili na maudhui ya vitendawili hivyo. Huku akiegemea misingi ya nadharia ya kijamii na ile ya kimuundo katika uchambuzi wake. Data zimepatikana kwa njia ya mahojiano na majadiliano ya vikundi lengwa na kuchambuliwa kwa njia yya maelezo kutoka katika makundi yote ya watafitiwa. Mshikamano huo umebainishwa kupitia vipengele anuai kama vile; mwelekeo wa kihistoria, kidini, kisiasa, kiuchumi, kimila na kadhalika. Umuhimu uliopo kwenye utafiti huu ni kwamba, katika utaratibu mzima wa kuvifahamu vitendawili panahitajika watu waangaze zaidi mshikamano wa sanaa na maudhui. Kwani sanaa ya vitendawili haikuwekwa kama mitindo tu ya lugha, bali imetomewa ndani yake maudhui maalumu. Hivyo jamii imeshauriwa kutoviangalia vipengele vya kifani na kimaudhui katika upekee wake, bali vichunguzwe katika mshikamano wake. Ndipo ladha ya vitendawili hivyo itakapopatikana. Maana ya wazi ambayo hujikita zaidi katika kutambulisha utamaduni wa vitu. Na maana fiche (ya ndani) ambayo hii hutambulisha utamaduni wa kifikra wa wanajamii husika. Pia kupitia hilo, kutajenga mtazamo mpya wa kuona thamani ya vitendawili kama taaluma maalumu, badala ya kuonekanwa kama mchezo wa watoto au chemsha bongo tu.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Mshikamano wa maudhui katika sanaa ya vitendawili
Citation