Vitendoneni Katika Hutuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka 2015, na Athari zake kwa Wanajamii wa Zanzibar
No Thumbnail Available
Date
2018-12
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu Umechunguza Vitendoneni Katika Hotuba za Kampeni za Uchaguzi za Mwaka, 2015 na Athari Zake kwa Wanajamii wa Zanzibar. Huu ni utafiti wa uwandani uliojumuisha matumizi ya mbinu shirikishi, usaili na maktabani katika kukusanya data na hatimaye data zimechambuliwa kwa njia ya kimaelezo na kitakwimu. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa. 1) Kubainisha vitendoneni vinavyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. 2) Kuchambua nia na nguvu za tamko kwa wazungumzaji kwenda kwa hadhirawanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. 3) Kuchambua athari hasi na chanya za vitendoneni kwa wanajamii wanaosikiliza hotuba za kampeni za uchaguziza Zanzibar. Utafiti huu umeongozwa na Nadharia ya Kitendoneni iliyoasisiwa na Austin, (1962) pamoja na Nadharia ya Umaanishiiliyoasisiwa na Grice (1975). Jumla ya vitendoneni athari vilikuwa, 120 ambapo vitendoneni vyenye mwelekeo chanya ni 90 ikiwa sawa na 75% na vitendoneni vyenye mwelekeo hasi ni 30 ikiwa sawa na 25%. Imegundulika kuwa vitendoneni vilivyojitokeza katika hotuba za kampeni za uchaguzi vina athari chanya na athari hasi kwa hadhira. Utafiti huu umeonesha kuwa, baadhi ya wazungumzaji wanatumia vitendoneni vinavyokiuka utaratibu wa mazungumzo na baadhi yake wanatumia vitendoneni vinavyozingatia utaratibu wa mazungumzo. Aidha imebainika kuwa yapo matamko ndani yake zimo kauli zisizokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Vile vile yapo matamko ambayo ndani yake zimo kauli zinazokubalika kutamkwa na wazungumzaji mbele ya hadhira. Mbali na hayo, wamekuwepo wazungumzaji wanaozingatia muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira na wanaokiuka muktadha wa mazungumzo mbele ya hadhira kiasi ya kuchangia mawazo yenye mtazamo hasi na mawazo yenye mtazamo chanya kwa hadhira. Pia imebainika kuwa yapo matamko ya hotuba ambayo ndani yake yanatumia kanuni za ushirikiano pamoja na kanuni za unyenyekevu.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Hutuba za kampeni za uchaguzi - Zanzibar 2. Athari za Hutuba za kampeni za uchaguzi - Zanzibar