Nafasi ya Kasida za Kiswahili Katika Kumtetea Mwanamke Zanzibar

No Thumbnail Available
Date
2018-12
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu umeshughulikia nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Kiini cha utafiti kimetokana na dhana kwamba baadhi ya watu katika jamii wanaamini kuwa kasida za Kiswahili hazina mchango wowote kwa jamii zaidi ya kuburudisha. Kutokana na hali hiyo, mtafiti alipata wazo la kufanya kazi hii baada ya kubaini kuwa hakuna utafiti wowote uliofanywa ukizihusisha kasida za Kiswahili katika utetezi wa mwanamke. Hivyo, utafiti huu umebainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili. Utafiti huu una lengo kuu moja ambalo ni kuchunguza nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Lengo hilo limekamilishwa na malengo mahsusi ambayo ni kubainissha kasida za Kiswahili zinazomtetea mwanamke, kubainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili na kutathmini nafasi ya kasida za Kiswahili kwa jamii ya wanawake . Dira iliyotumika kuongoza utafiti huu ni nadhariya ya ufeministi wa Kiislamu. Mbinu za utafiti zilizotumika katika kazi hii, ni pamoja na mbinu ya maktabani, uwandani, mbinu za mahojiano ya ana kwa ana na watafitiwa na mbinu ya uchunguzi shirikishi uliofanywa katika sehemu ambazo kasida huwasilishwa. Utafiti umebainisha kuwa zipo baadhi ya kasida za Kiswahil zenye utetezi wa mwanamke. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwepo kwa utetezi wa mwanamke katika nyanja za kijamii, kielimu, kiuchumi na kisiasa. Utafiti umebaini kuwa, kasida zinamtetea mwanamke zaidi katika suala la ndoa. Utetezi wa mwanamke uliobainika katika kasida ni pamoja kuthaminiwa idhini ya mwanamke katika ndoa. Na mwanamke kupewa nafasi ya kuchagua mchumba
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Utetezi wa mwanamke - Zanzibar 2. Nafasi ya mwanamke katika jamii 3. Kasida na mwanamke wa kizanzibar
Citation