Nafasi ya Kasida za Kiswahili Katika Kumtetea Mwanamke Zanzibar

dc.contributor.authorHAMAD, Kombo Sharif
dc.date.accessioned2020-08-18T08:33:20Z
dc.date.available2020-08-18T08:33:20Z
dc.date.issued2018-12
dc.descriptionAvailable in print form, Tunguu Reference Libraryen_US
dc.description.abstractUtafiti huu umeshughulikia nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Kiini cha utafiti kimetokana na dhana kwamba baadhi ya watu katika jamii wanaamini kuwa kasida za Kiswahili hazina mchango wowote kwa jamii zaidi ya kuburudisha. Kutokana na hali hiyo, mtafiti alipata wazo la kufanya kazi hii baada ya kubaini kuwa hakuna utafiti wowote uliofanywa ukizihusisha kasida za Kiswahili katika utetezi wa mwanamke. Hivyo, utafiti huu umebainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili. Utafiti huu una lengo kuu moja ambalo ni kuchunguza nafasi ya kasida za Kiswahili katika kumtetea mwanamke. Lengo hilo limekamilishwa na malengo mahsusi ambayo ni kubainissha kasida za Kiswahili zinazomtetea mwanamke, kubainisha utetezi wa mwanamke katika nyanja mbalimbali kupitia kasida za Kiswahili na kutathmini nafasi ya kasida za Kiswahili kwa jamii ya wanawake . Dira iliyotumika kuongoza utafiti huu ni nadhariya ya ufeministi wa Kiislamu. Mbinu za utafiti zilizotumika katika kazi hii, ni pamoja na mbinu ya maktabani, uwandani, mbinu za mahojiano ya ana kwa ana na watafitiwa na mbinu ya uchunguzi shirikishi uliofanywa katika sehemu ambazo kasida huwasilishwa. Utafiti umebainisha kuwa zipo baadhi ya kasida za Kiswahil zenye utetezi wa mwanamke. Aidha, matokeo ya utafiti huu yamebainisha kuwepo kwa utetezi wa mwanamke katika nyanja za kijamii, kielimu, kiuchumi na kisiasa. Utafiti umebaini kuwa, kasida zinamtetea mwanamke zaidi katika suala la ndoa. Utetezi wa mwanamke uliobainika katika kasida ni pamoja kuthaminiwa idhini ya mwanamke katika ndoa. Na mwanamke kupewa nafasi ya kuchagua mchumbaen_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/151
dc.language.isootheren_US
dc.publisherThe State University of Zanzibar (SUZA)en_US
dc.subject1. Utetezi wa mwanamke - Zanzibar 2. Nafasi ya mwanamke katika jamii 3. Kasida na mwanamke wa kizanzibaren_US
dc.titleNafasi ya Kasida za Kiswahili Katika Kumtetea Mwanamke Zanzibaren_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
TASNIFU - KOMBO.pdf
Size:
875.18 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: