Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa:
No Thumbnail Available
Date
2018-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Utafiti huu unahusu ‘Usasa wa Mashairi ya Nyimbo za Taarab ya Sasa’. Mashairi ya nyimbo
kadhaa wa kadhaa za taarab yamechunguzwa. Uchunguzi ulianzia na mashairi ya nyimbo za
taarab halisi ambayo yametumika kama kigezo msingi katika kutambulisha usasa wa mashairi
ya taarab ya sasa. Utafiti umefanyika katika wilaya tatu za Tanzania Visiwani na wilaya mbili
za Tanzania Bara. Kwa upande wa visiwani ni Wilaya ya Chake Chake iliyopo Mkoa wa
Kusini Pemba, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba na Wilaya ya Mjini katika Mkoa
wa Mjini Magharibi, Unguja. Kwa Bara, ni Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Kinondoni,
Daressalaam. Malengo ya utafiti huu yalikuwa matano. La kwanza, kuainisha sifa bainifu za
mashairi ya taarab halisi. La pili ni kudhihirisha mambo yaliyobadilika katika mashairi ya
taarab ya sasa. La tatu ni kupambanua sababu za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La
nne, kutathmini athari za mabadiliko ya mashairi ya taarab ya sasa. La tano ni kuchunguza
namna wasanii na wapenzi wa nyimbo za taarab wanavyoyapokea mabadiliko ya fani na
maudhui yaliyomo kwenye mashairi ya taarab ya sasa. Data ilipatikana kupitia mbinu ya
ushiriki nafsia, mbinu ya mahojiano, mbinu ya dodoso na mbinu ya kuwa na mtafiti msaidizi.
Pamoja na mbinu hizo utafiti ulitumia Nadharia ya Uamilifu, Nadharia ya Semiotiki na
Unadharia Unaozama, pamoja na Mkabala wa Utafsiriji wa Vitendo na Mkabala wa Kiislamu.
Watafitiwa walikuwa watunzi wa mashairi, waimbaji, wapiga ala za muziki pamoja na
washabiki/wapenzi wa muziki wa taarab. Uchambuzi wa data umeonesha kuwa ni kweli
kabisa kwamba pana usasa wa waziwazi kwenye mashairi katika taarab ya sasa. Usasa huo
ndio msingi uliyoshusha hadhi ya mashairi ya taarab ya sasa na kuwa maneno tu. Vile vile,
muziki huo utambulikanao kama taarab ya sasa wakosa vigezo thabiti vyenye kuyakinisha
uhalali wa kuitwa taarab.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Sifa bainifu za mashairi ya taarab halisi 2. Mabadiliko katika mashairi ya taarab ya sasa - Sababu na athari