UBADILISHAJI MSIMBO KATIKA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI
Loading...
Date
2020-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili
kwa wageni. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ubadilishaji msimbo katika
kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni. Malengo mahususi ya utafiti huu ni
kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za
ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha
na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili
ambazo ni Nadharia kidhi ya mawasiliano ya Giles (1979) na Nadharia ya umaanisho
ya Grice (1975). Utafiti umehusisha jumla ya Watoa taarifa 34 wakiwemo walimu
wanaofundisha wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili, wanafunzi
wanaojifunza kufundisha Kiswahili kwa wageni na wanafunzi wa kigeni
wanaojifunza Kiswahili. Utafiti huu umefuata mkabala wa kimaelezo. Taarifa za
utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti
umegundua kwamba msimbo sentensi umejitokeza zaidi katika kufundisha na
kujifunza Kiswahili kwa wageni. Pia utafiti umegundua kuwa zipo sababu
mbalimbali zinazosababisha ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza
Kiswahili kwa wageni ambazo ni kurahisisha somo, umilisi wa lugha zaidi ya moja
na kufafanua msamiati mpya. Aidha, utafiti umegundua kwamba zipo athari chanya
na hasi za ubadilishaji msimbo. Athari chanya ni kuimarisha ufahamu wa wanafunzi
na wanafunzi kushiriki vizuri katika somo. Athari hasi zilizobainika ni pamoja na
kumchanganya mwanafunzi, kutokuelewana kati ya mwalimu na mwanafunzi,
kuchochea ubaguzi, kuvunja kanuni ya ufundishaji wa lugha ya kigeni na kuzoea
maneno ya Kiingereza kuliko ya Kiswahili. Kutokana na uwepo wa athari nyingi hasi
za ubadilishaji msimbo, mtafiti anahitimisha kwamba ubadilishaji msimbo katika
kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni si jambo sahihi. Hivyo utafiti huu
unapendekeza kwamba, kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni hauna budi
kutumia lugha lengwa (Kiswahili)
Description
Malengo mahususi ya utafiti huu ni kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za
ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni