UBADILISHAJI MSIMBO KATIKA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI

dc.contributor.authorMOHAMMED,Saida Salum
dc.date.accessioned2024-04-02T08:26:18Z
dc.date.available2024-04-02T08:26:18Z
dc.date.issued2020-12-01
dc.descriptionMalengo mahususi ya utafiti huu ni kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ubadilishaji msimbo katika kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni. Malengo mahususi ya utafiti huu ni kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia kidhi ya mawasiliano ya Giles (1979) na Nadharia ya umaanisho ya Grice (1975). Utafiti umehusisha jumla ya Watoa taarifa 34 wakiwemo walimu wanaofundisha wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili, wanafunzi wanaojifunza kufundisha Kiswahili kwa wageni na wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili. Utafiti huu umefuata mkabala wa kimaelezo. Taarifa za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti umegundua kwamba msimbo sentensi umejitokeza zaidi katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Pia utafiti umegundua kuwa zipo sababu mbalimbali zinazosababisha ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni ambazo ni kurahisisha somo, umilisi wa lugha zaidi ya moja na kufafanua msamiati mpya. Aidha, utafiti umegundua kwamba zipo athari chanya na hasi za ubadilishaji msimbo. Athari chanya ni kuimarisha ufahamu wa wanafunzi na wanafunzi kushiriki vizuri katika somo. Athari hasi zilizobainika ni pamoja na kumchanganya mwanafunzi, kutokuelewana kati ya mwalimu na mwanafunzi, kuchochea ubaguzi, kuvunja kanuni ya ufundishaji wa lugha ya kigeni na kuzoea maneno ya Kiingereza kuliko ya Kiswahili. Kutokana na uwepo wa athari nyingi hasi za ubadilishaji msimbo, mtafiti anahitimisha kwamba ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni si jambo sahihi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba, kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni hauna budi kutumia lugha lengwa (Kiswahili)
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherTHESIS
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/203
dc.language.isoen
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries00001; 2020
dc.titleUBADILISHAJI MSIMBO KATIKA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
UBADILISHAJI MSIMBO KATIKA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI.pdf
Size:
435.87 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: