UBADILISHAJI MSIMBO KATIKA KUJIFUNZA NA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI

No Thumbnail Available
Date
2020-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Lengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza ubadilishaji msimbo katika kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni. Malengo mahususi ya utafiti huu ni kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu umeongozwa na nadharia mbili ambazo ni Nadharia kidhi ya mawasiliano ya Giles (1979) na Nadharia ya umaanisho ya Grice (1975). Utafiti umehusisha jumla ya Watoa taarifa 34 wakiwemo walimu wanaofundisha wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili, wanafunzi wanaojifunza kufundisha Kiswahili kwa wageni na wanafunzi wa kigeni wanaojifunza Kiswahili. Utafiti huu umefuata mkabala wa kimaelezo. Taarifa za utafiti huu zimekusanywa kwa kutumia mbinu za mahojiano na ushuhudiaji. Utafiti umegundua kwamba msimbo sentensi umejitokeza zaidi katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni. Pia utafiti umegundua kuwa zipo sababu mbalimbali zinazosababisha ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni ambazo ni kurahisisha somo, umilisi wa lugha zaidi ya moja na kufafanua msamiati mpya. Aidha, utafiti umegundua kwamba zipo athari chanya na hasi za ubadilishaji msimbo. Athari chanya ni kuimarisha ufahamu wa wanafunzi na wanafunzi kushiriki vizuri katika somo. Athari hasi zilizobainika ni pamoja na kumchanganya mwanafunzi, kutokuelewana kati ya mwalimu na mwanafunzi, kuchochea ubaguzi, kuvunja kanuni ya ufundishaji wa lugha ya kigeni na kuzoea maneno ya Kiingereza kuliko ya Kiswahili. Kutokana na uwepo wa athari nyingi hasi za ubadilishaji msimbo, mtafiti anahitimisha kwamba ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni si jambo sahihi. Hivyo utafiti huu unapendekeza kwamba, kujifunza na kufundisha Kiswahili kwa wageni hauna budi kutumia lugha lengwa (Kiswahili)
Description
Malengo mahususi ya utafiti huu ni kubainisha aina ya ubadilishaji msimbo inayojitokeza zaidi, kufafanua sababu za ubadilishaji msimbo na kutathmini athari za ubadilishaji msimbo katika kufundisha na kujifunza Kiswahili kwa wageni
Keywords
Citation