MKABALA UNAOTUMIKA KATIKA UTUNGAJI WA MITIHANI YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI:
Loading...
Date
2020-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu Mkabala Unaotumika Katika Utungaji wa Mitihani ya Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni: Mfano Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu. Kwanza kufafanuakwa kiasi gani walimu wanaotunga maswali ya mitihani ya Kiswahili kwa wageni wanavyoifahamu mikabala ya utungaji mitihani. Pilikubainisha aina ya mkabala unaotumika zaidi katika utungaji wa maswali ya mitihani ya Kiswahili kw wageni. Tatu kuchunguza mtazamo wa walimu juu ya mkabala wanaoutumia zaidi katika utungaji wa maswali ya mitihani ya Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu ulifanywa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ilikuwa Nadhari ya Tabia ya Umoja (Unitary Trait Hypothesis) kama ilivyoasisiwa na Oller (1979).Misingi mikuu ya nadharia hii ni kuipima lugha kwa njia ya mjumuishi pamoja na uzingatiaji wa mazingira halisi ya watumiaji wa lugha inayohusika wakati wa upimwaji wake.Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni walimu saba wanaosomesha Kiswahili kwa wageni, watoa taarifa hao walipatikana kwa usampulishaji tajwa. Mbinu
zilizotumika ni mbinu ya dodoso kwa ajili ya kukusanya data za lengo la kwanza hadilengo la tatu, na mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika kwa ajili ya kukusanya data za lengo la pili tu la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalieleza kwamba walimu wanaosomesha Kiswahili kwa wageni wanaufahamuwa mikabala ya utungaji mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa asilimia 57%. Pia utafiti ulionesha kwamba mkabala unaopima stadi nyingi za lugha kwa wakati mmoja ndio ambao hutumika zaidi, na mtazamo wa walimu kuhusu mkabala unaotumika zaidikwamujibu wa matokeo ya
utafiti ni wenye kufaa kwani unawapatia matokeo wanayoyahitaji katika upimaji wa
Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulitoa mapendekezo ya kwamba walimu
waongeze taaluma yao juu ya mikabala ya upimaji, pamoja na uzingatiaji wa stadi
zotekuunne za lugha katika upimaji wa wanafunzi ili kuhakikisha kwamba hakuna stadi
ya lugha hata moja ambayoinaachwa nyuma wakati wa upimaji wa wanafunzi.
Description
Misingi mikuu ya nadharia hii ni kuipima lugha kwa njia ya mjumuishi pamoja na uzingatiaji wa mazingira halisi ya watumiaji wa lugha inayohusika wakati wa upimwaji wake.Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni walimu saba wanaosomesha Kiswahili kwa wageni, watoa taarifa hao walipatikana kwa usampulishaji tajwa. Mbinu zilizotumika ni mbinu ya dodoso kwa ajili ya kukusanya data za lengo