MKABALA UNAOTUMIKA KATIKA UTUNGAJI WA MITIHANI YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI:

dc.contributor.authorMGASHO,Makame Sheha
dc.date.accessioned2024-05-29T06:14:30Z
dc.date.available2024-05-29T06:14:30Z
dc.date.issued2020-12-01
dc.descriptionMisingi mikuu ya nadharia hii ni kuipima lugha kwa njia ya mjumuishi pamoja na uzingatiaji wa mazingira halisi ya watumiaji wa lugha inayohusika wakati wa upimwaji wake.Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni walimu saba wanaosomesha Kiswahili kwa wageni, watoa taarifa hao walipatikana kwa usampulishaji tajwa. Mbinu zilizotumika ni mbinu ya dodoso kwa ajili ya kukusanya data za lengo
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu Mkabala Unaotumika Katika Utungaji wa Mitihani ya Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni: Mfano Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi matatu. Kwanza kufafanuakwa kiasi gani walimu wanaotunga maswali ya mitihani ya Kiswahili kwa wageni wanavyoifahamu mikabala ya utungaji mitihani. Pilikubainisha aina ya mkabala unaotumika zaidi katika utungaji wa maswali ya mitihani ya Kiswahili kw wageni. Tatu kuchunguza mtazamo wa walimu juu ya mkabala wanaoutumia zaidi katika utungaji wa maswali ya mitihani ya Kiswahili kwa wageni. Utafiti huu ulifanywa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ilikuwa Nadhari ya Tabia ya Umoja (Unitary Trait Hypothesis) kama ilivyoasisiwa na Oller (1979).Misingi mikuu ya nadharia hii ni kuipima lugha kwa njia ya mjumuishi pamoja na uzingatiaji wa mazingira halisi ya watumiaji wa lugha inayohusika wakati wa upimwaji wake.Sampuli ya utafiti huu ilikuwa ni walimu saba wanaosomesha Kiswahili kwa wageni, watoa taarifa hao walipatikana kwa usampulishaji tajwa. Mbinu zilizotumika ni mbinu ya dodoso kwa ajili ya kukusanya data za lengo la kwanza hadilengo la tatu, na mbinu ya uchambuzi wa nyaraka ilitumika kwa ajili ya kukusanya data za lengo la pili tu la utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalieleza kwamba walimu wanaosomesha Kiswahili kwa wageni wanaufahamuwa mikabala ya utungaji mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni kwa asilimia 57%. Pia utafiti ulionesha kwamba mkabala unaopima stadi nyingi za lugha kwa wakati mmoja ndio ambao hutumika zaidi, na mtazamo wa walimu kuhusu mkabala unaotumika zaidikwamujibu wa matokeo ya utafiti ni wenye kufaa kwani unawapatia matokeo wanayoyahitaji katika upimaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu ulitoa mapendekezo ya kwamba walimu waongeze taaluma yao juu ya mikabala ya upimaji, pamoja na uzingatiaji wa stadi zotekuunne za lugha katika upimaji wa wanafunzi ili kuhakikisha kwamba hakuna stadi ya lugha hata moja ambayoinaachwa nyuma wakati wa upimaji wa wanafunzi.
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherMETK/2/2018/03/TZ
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/295
dc.language.isoother
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries00001; 2020
dc.titleMKABALA UNAOTUMIKA KATIKA UTUNGAJI WA MITIHANI YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI:
dc.title.alternativeMfano Chuo Kikuu Cha Taifa Cha Zanzibar
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MKABALA UNAOTUMIKA KATIKA UTUNGAJI WA MITIHANI YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI.pdf
Size:
704.03 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: