Matumizi ya Viamsha Darasa Katika Ufundishaji wa Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni
Loading...
Date
2021-03-12
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulilenga kuchunguza matumizi ya viamsha darasa katika ufundishaji wa
Kiswahili kama lugha ya kigeni. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni kubainisha viamsha
darasa vinavyotumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni, kufafanua
namna gani viamsha darasa vinatumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni
na kuelezea athari za viamsha darasa katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni.
Masuali ya utafiti huu ni viamsha darasa gani hutumika wakati wa ufundishaji wa
Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha
darasa hutumikaje wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha darasa vina athari gani wakati wa ufundishaji wa
Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar?. Utafiti huu
ulifanywa Zanzibar katika kisiwa cha Unguja katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
- Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Watoa taarifa wa utafiti huu walikuwa walimu wazoefu
na wanafunzi wa Kiswahili kwa wageni wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika
Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Elimu ya Binaadamu
iliyoasisiwa katikati ya karne ya ishirini na Erik Erikson (1963, 1968), Abraham Maslow
(1968, 1970) Carl Rogers (1969); Arthur, W. Comb (1970), George Isaac Brown (1975)
na wengineo. Utafiti huu ulitumia mahojiano na ushuhudiaji kama ni mbinu za kukusanyia
wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa kuna baadhi ya walimu hutumia kiamsha
darasa cha mazungumzo mwanzo wa kipindi tu na walimu wengine hutumia viamsha
darasa mbalimbali mwanzo na katikati ya kipindi kwa lengo la kuleta ufanisi katika
mchakato mzima wa ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni. Pendekezo kwa walimu
wa Kiswahili wageni ni kuwa wabunifu wa kuviandaa na kuvitumia viamsha darasa
wakati wote wa mchakato wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni kulingana
na hali ya mwanafunzi, kiwango cha mwanafunzi, raghaba ya mwanafunzi, utayari wa
mwanafunzi na hata jinsia ya mwanafunzi
Description
Malengo mahsusi ya utafiti huu ni kubainisha viamsha darasa vinavyotumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni, kufafanua namna gani viamsha darasa vinatumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuelezea athari za viamsha darasa katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni