Matumizi ya Viamsha Darasa Katika Ufundishaji wa Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni

dc.contributor.authorABUBAKAR,Fatma Saleh
dc.date.accessioned2024-04-02T08:50:18Z
dc.date.available2024-04-02T08:50:18Z
dc.date.issued2021-03-12
dc.descriptionMalengo mahsusi ya utafiti huu ni kubainisha viamsha darasa vinavyotumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni, kufafanua namna gani viamsha darasa vinatumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuelezea athari za viamsha darasa katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni
dc.description.abstractUtafiti huu ulilenga kuchunguza matumizi ya viamsha darasa katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni kubainisha viamsha darasa vinavyotumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni, kufafanua namna gani viamsha darasa vinatumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuelezea athari za viamsha darasa katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni. Masuali ya utafiti huu ni viamsha darasa gani hutumika wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha darasa hutumikaje wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha darasa vina athari gani wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar?. Utafiti huu ulifanywa Zanzibar katika kisiwa cha Unguja katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar - Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Watoa taarifa wa utafiti huu walikuwa walimu wazoefu na wanafunzi wa Kiswahili kwa wageni wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Elimu ya Binaadamu iliyoasisiwa katikati ya karne ya ishirini na Erik Erikson (1963, 1968), Abraham Maslow (1968, 1970) Carl Rogers (1969); Arthur, W. Comb (1970), George Isaac Brown (1975) na wengineo. Utafiti huu ulitumia mahojiano na ushuhudiaji kama ni mbinu za kukusanyia wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa kuna baadhi ya walimu hutumia kiamsha darasa cha mazungumzo mwanzo wa kipindi tu na walimu wengine hutumia viamsha darasa mbalimbali mwanzo na katikati ya kipindi kwa lengo la kuleta ufanisi katika mchakato mzima wa ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni. Pendekezo kwa walimu wa Kiswahili wageni ni kuwa wabunifu wa kuviandaa na kuvitumia viamsha darasa wakati wote wa mchakato wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni kulingana na hali ya mwanafunzi, kiwango cha mwanafunzi, raghaba ya mwanafunzi, utayari wa mwanafunzi na hata jinsia ya mwanafunzi
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherTHESIS
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/204
dc.language.isoen
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries00001; 2021
dc.titleMatumizi ya Viamsha Darasa Katika Ufundishaji wa Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
UTAFITI-VIAMSHADARASA-FINAL DRAFT.pdf
Size:
775.64 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: