MATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA
Loading...
Date
2022-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa
za promosheni majumbani. Utafiti ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi „B‟ Kisiwani
Unguja na kuhusisha kampuni ya Progressive Marketing Company Limited na Sumbezi
Marketing Directing. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya
upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa
na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole
inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na
wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya
upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Jumla ya
watoataarifa 29 walihusishwa katika utafiti huu. Mazungumzo kumi (10) ya kimaandishi
yalichanganuliwa ili kupata data ya mikakati ya upole kukidhi lengo la kwanza. Data
hiyo ilipatikana kupitia mbinu ya ushuhudiaji, hata hivyo mbinu ya mahojiano ilitumika
kupata maoni yaliyolikamilisha lengo la pili. Hatimaye uchanganuzi wa data ulifanywa
kwa kutumia mkabala wa kimaelezo.Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole ya Brown
na Levinson (1987). Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wauza bidhaa za
promosheni majumbani hutumia mikakati minne ya upole yaani; mkakati wa
kuzungumza kwa uwazi, mkakati wa upole chanya, mkakati wa upole hasi na mkakati
wa kuzungumza kwa kuficha katika mazungumzo yao wakati wanapoamiliana na wateja
wao. Halikadhalika kupitia data ya maoni, wasailiwa walikiri kuwa matumizi ya lugha
ya upole husaidia kujenga heshima, kukuza mahusiano mazuri baina ya wauzaji na
wanunuzi na kuongeza mauzo katika biashara yao. Kwa ujumla, utafiti unapendekeza
kufanyika kwa tafiti zaidi zitakazobainisha vipengele vya kilughawiya vinavyounda
lugha ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.
Description
Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya
upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa
na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole
inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na
wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya
upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.