MATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA

dc.contributor.authorALI,Maryam Kombo
dc.date.accessioned2024-04-02T08:09:26Z
dc.date.available2024-04-02T08:09:26Z
dc.date.issued2022-12-01
dc.descriptionLengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulifanywa katika Wilaya ya Magharibi „B‟ Kisiwani Unguja na kuhusisha kampuni ya Progressive Marketing Company Limited na Sumbezi Marketing Directing. Lengo la utafiti huu lilikuwa ni kuchunguza matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Utafiti ulikuwa na malengo mahsusi mawili. Lengo la kwanza lilikuwa ni kufafanua mikakati ya upole inayotumiwa na wauza bidhaa za promosheni majumbani katika mazungumzo yao na wateja wao. Na lengo la pili lilikuwa ni kuchambua athari ya matumizi ya lugha ya upole katika mazungumzo ya wauza bidhaa za promosheni majumbani. Jumla ya watoataarifa 29 walihusishwa katika utafiti huu. Mazungumzo kumi (10) ya kimaandishi yalichanganuliwa ili kupata data ya mikakati ya upole kukidhi lengo la kwanza. Data hiyo ilipatikana kupitia mbinu ya ushuhudiaji, hata hivyo mbinu ya mahojiano ilitumika kupata maoni yaliyolikamilisha lengo la pili. Hatimaye uchanganuzi wa data ulifanywa kwa kutumia mkabala wa kimaelezo.Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Upole ya Brown na Levinson (1987). Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba wauza bidhaa za promosheni majumbani hutumia mikakati minne ya upole yaani; mkakati wa kuzungumza kwa uwazi, mkakati wa upole chanya, mkakati wa upole hasi na mkakati wa kuzungumza kwa kuficha katika mazungumzo yao wakati wanapoamiliana na wateja wao. Halikadhalika kupitia data ya maoni, wasailiwa walikiri kuwa matumizi ya lugha ya upole husaidia kujenga heshima, kukuza mahusiano mazuri baina ya wauzaji na wanunuzi na kuongeza mauzo katika biashara yao. Kwa ujumla, utafiti unapendekeza kufanyika kwa tafiti zaidi zitakazobainisha vipengele vya kilughawiya vinavyounda lugha ya wauza bidhaa za promosheni majumbani.
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherTHESIS
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/202
dc.language.isoen
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries00001; 2022
dc.titleMATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
MATUMIZI YA LUGHA YA UPOLE KATIKA MAZUNGUMZO YA WAUZA BIDHAA ZA PROMOSHENI MAJUMBANI KISIWANI UNGUJA. pdf
Size:
2.23 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: