Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Subject "1. Ulinganishi wa Lahaja - Kipemba, Kiumbatu na Kimakunduchi"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
- ItemUlinganishi wa Njeo na Hali kaika Lahaje za Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi(The State University of Zanzibar (SUZA), 2018-01) HAMAD, Salma OmarUtafiti huu umelenga kulinganisha uwakilishaji wa njeo na hali katika lahaja za Kipemba (KP), Kitumbatu (KT) na Kimakunduchi (KM) kwa kuzingatia maumbo ya vitenzi vya lahaja hizi. Lengo hili limefikiwa kwa kupitia malengo mahususi ambayo ni kubainisha mofimu za njeo na hali katika KP, kubainisha mofimu za njeo na hali katika KT, kubainisha mofimu za njeo na hali katika KM na kufafanua kufanana na kutafautiana kwa lahaja hizo katika uwakilishaji wa njeo na hali. Utafiti huu umeongozwa na nadharia ya utambuzi ya Guillaume (1965) na nadharia ya Fonolojia Zalishi ya Chomsky na Halle (1968). Data za utafiti huu zimekusanywa kwa mbinu ya kusoma maandiko, usaili na uchunguzi. Utafiti huu umebaini kwamba lahaja zote tatu zilizotafitiwa zina idadi sawa ya aina za njeo na hali. Katika uwakilishaji wa njeo na hali hizo, kuna baadhi ya maumbo ya mofimu yamefanana kwa lahaja zote tatu, baadhi yamefanana kati ya KM na KT na baadhi yamefanana kati ya KT na KP. Hata hivyo, tukiachana na maumbo ya mofimu yaliyofanana kwa lahaja zote tatu, hakujajitokeza umbo jingine lolote la mofimu lililofanana kati ya KM na KP. Hali hii inasababisha mfanano kuwa mkubwa kati ya KM na KT na pia kati ya KT na KP huku kukiwa na tafauti kubwa kati ya KM na KP katika vipengele hivi vya kimofosintaksia na kimofosintasematiki vya uwakilishaji wa njeo na hali. Mtafiti amependekeza tafiti zaidi zifanyike katika kipengele cha njeo na hali kwa lahaja zote za Kiswahili ili kubaini lahaja zipi zinafanana na zipi zinatafautiana miongoni mwa lahaja hizo. Aidha, kuna haja ya kutafiti kwa kina sababu ya mfanano na tafauti hizo.