Thesis and dissertation
Permanent URI for this collection
Browse
Browsing Thesis and dissertation by Author "ABUBAKAR,Fatma Saleh"
Now showing 1 - 1 of 1
Results Per Page
Sort Options
- ItemMatumizi ya Viamsha Darasa Katika Ufundishaji wa Kiswahili Kama Lugha ya Kigeni(SUZA, 2021-03-12) ABUBAKAR,Fatma SalehUtafiti huu ulilenga kuchunguza matumizi ya viamsha darasa katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni. Malengo mahsusi ya utafiti huu ni kubainisha viamsha darasa vinavyotumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni, kufafanua namna gani viamsha darasa vinatumika katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuelezea athari za viamsha darasa katika ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni. Masuali ya utafiti huu ni viamsha darasa gani hutumika wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha darasa hutumikaje wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar? viamsha darasa vina athari gani wakati wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar?. Utafiti huu ulifanywa Zanzibar katika kisiwa cha Unguja katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar - Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Watoa taarifa wa utafiti huu walikuwa walimu wazoefu na wanafunzi wa Kiswahili kwa wageni wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni. Utafiti huu ulitumia nadharia ya Elimu ya Binaadamu iliyoasisiwa katikati ya karne ya ishirini na Erik Erikson (1963, 1968), Abraham Maslow (1968, 1970) Carl Rogers (1969); Arthur, W. Comb (1970), George Isaac Brown (1975) na wengineo. Utafiti huu ulitumia mahojiano na ushuhudiaji kama ni mbinu za kukusanyia wa data. Matokeo ya utafiti huu yalibaini kuwa kuna baadhi ya walimu hutumia kiamsha darasa cha mazungumzo mwanzo wa kipindi tu na walimu wengine hutumia viamsha darasa mbalimbali mwanzo na katikati ya kipindi kwa lengo la kuleta ufanisi katika mchakato mzima wa ufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni. Pendekezo kwa walimu wa Kiswahili wageni ni kuwa wabunifu wa kuviandaa na kuvitumia viamsha darasa wakati wote wa mchakato wa ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni kulingana na hali ya mwanafunzi, kiwango cha mwanafunzi, raghaba ya mwanafunzi, utayari wa mwanafunzi na hata jinsia ya mwanafunzi