Ulinganishaji wa Mofolojia ya Uambishaji wa Vitenzi Kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu

dc.contributor.authorJuma, Mwanahija Ali
dc.date.accessioned2021-12-20T09:12:59Z
dc.date.available2021-12-20T09:12:59Z
dc.date.issued2019-12
dc.descriptionTasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo.en_US
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo. Kimakunduchi ni lahaja inayozungumzwa kusini ya kisiwa cha Unguja kilichopo Zanzibar nchini Tanzania. Kitumbatu ni lahaja inayozungumzwa kaskazini ya kisiwa cha Unguja kilichopo Zanzibar Tanzania na Kiswahili sanifu ni lahaja iliyosanifiwa na kutumika katika maeneo yote rasmi popote duniani. Lahaja hizi tatu zina vitenzi vyenye viambishi kabla na baada ya mzizi wa kitenzi. Katika utafiti huu tumeshughulikia viambishi vya nafsi, viambishi vya njeo na viambishi vya yambwa. Kazi hii imetumia nadharia ya Umbo Upeo katika kubainisha mofolojia ya vitenzi, kufafanua mashartizuizi ya viambishi na kuyalinganisha katika Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Utafiti umebaini kuwapo kwa mlingano mkubwa wa mashartizuizi kati ya Kimakunduchi na Kitumbatu, pia mlingano kwa kiasi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu na tofauti chache kati ya lahaja hizo. Nadharia ya Umbo Upeo inashughulikia masuala ya kifonolojia ambayo yalionekana kujitokeza katika muundo wa sauti. Hata hivyo baadae nadharia hii imetumika katika kushughulikia masuala mengine ya kiisimu kama vile sintaksia, semantiki, mofolojia, isimujamii, isimu historia na taaluma nyingine kwa lengo la kuvibainisha vipengele vya kiisimu vilivyomo katika matawi hayo ya kiisimu kwa kuzingatia misingi mitatu ambayo ni Uzalishaji, Mashartizuizi na Tathmiini. Vilevile, huangalia jinsi lugha inavyopokea na kuzalisha vipashio mbalimbali vikiwemo mofu na kuvibainisha mashartizuizi yake na mwisho kuvifanyia tathmini kwa kuangalia ukubalifu, uhafifu au kutokukubalika kwa vipengele hivyo katika lugha inayohusikaen_US
dc.description.sponsorshipTHE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBARen_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/180
dc.language.isootheren_US
dc.publisherTHE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBARen_US
dc.titleUlinganishaji wa Mofolojia ya Uambishaji wa Vitenzi Kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifuen_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
TASNIFU FULL BINDING -MWANAHIJA FINAL.pdf
Size:
3.26 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
Tasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo.
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: