Ulinganishaji wa Mofolojia ya Uambishaji wa Vitenzi Kati ya Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu
No Thumbnail Available
Date
2019-12
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
THE STATE UNIVERSITY OF ZANZIBAR
Abstract
Tasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya
Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi
ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya
lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo. Kimakunduchi ni lahaja
inayozungumzwa kusini ya kisiwa cha Unguja kilichopo Zanzibar nchini Tanzania.
Kitumbatu ni lahaja inayozungumzwa kaskazini ya kisiwa cha Unguja kilichopo
Zanzibar Tanzania na Kiswahili sanifu ni lahaja iliyosanifiwa na kutumika katika
maeneo yote rasmi popote duniani. Lahaja hizi tatu zina vitenzi vyenye viambishi
kabla na baada ya mzizi wa kitenzi. Katika utafiti huu tumeshughulikia viambishi
vya nafsi, viambishi vya njeo na viambishi vya yambwa. Kazi hii imetumia nadharia
ya Umbo Upeo katika kubainisha mofolojia ya vitenzi, kufafanua mashartizuizi ya
viambishi na kuyalinganisha katika Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu.
Utafiti umebaini kuwapo kwa mlingano mkubwa wa mashartizuizi kati ya
Kimakunduchi na Kitumbatu, pia mlingano kwa kiasi kati ya Kimakunduchi,
Kitumbatu na Kiswahili Sanifu na tofauti chache kati ya lahaja hizo. Nadharia ya
Umbo Upeo inashughulikia masuala ya kifonolojia ambayo yalionekana kujitokeza
katika muundo wa sauti. Hata hivyo baadae nadharia hii imetumika katika
kushughulikia masuala mengine ya kiisimu kama vile sintaksia, semantiki,
mofolojia, isimujamii, isimu historia na taaluma nyingine kwa lengo la kuvibainisha
vipengele vya kiisimu vilivyomo katika matawi hayo ya kiisimu kwa kuzingatia
misingi mitatu ambayo ni Uzalishaji, Mashartizuizi na Tathmiini. Vilevile, huangalia
jinsi lugha inavyopokea na kuzalisha vipashio mbalimbali vikiwemo mofu na
kuvibainisha mashartizuizi yake na mwisho kuvifanyia tathmini kwa kuangalia
ukubalifu, uhafifu au kutokukubalika kwa vipengele hivyo katika lugha inayohusika
Description
Tasnifu hii inahusu ulinganishi wa mofolojia ya uambishaji wa vitenzi kati ya
Kimakunduchi, Kitumbatu na Kiswahili Sanifu. Mofolojia ya uambishaji wa vitenzi
ni miongoni mwa vipengele vya sarufi vinavyojihusisha na uchambuzi wa sayansi ya
lugha kwa kubainisha na kufafanua vipashio vya kimaumbo.