USAHIHISHAJI WA MAKOSA YA KISARUFI KATIKA STADI YA KUZUNGUMZA KATIKA DARASA LA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI
Loading...
Date
2020-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu usahihishaji wa makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza
katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu umefanyika katika Chuo
Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika kampasi ya Vuga, Zanzibar. Malengo ya
utafiti huu ni kubainisha makosa ya kisarufi ambayo walimu wanayasahihisha zaidi
katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni, kueleza
mbinu ambazo walimu wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika
stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni na kufafanua
mitazamo ya walimu juu ya mbinu wanazozipendelea kutumia katika kusahihisha
makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha
ya kigeni. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiwa na Corder (1967) imetumika
kuongozea utafiti huu. Data za msingi zimepatikana kwa njia ya ushuhudiaji,
mahojiano na majadiliano. Watoa taarifa walikuwa ni walimu wanane wanaofundisha
Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha awali na kiwango cha kati.
Matokeo yameonesha makosa ya kisarufi ambayo walimu wameyasahihisha zaidi
katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni ni
makosa ya mpangilio wa vipashio usiostahiki, njeo, upatanisho wa kisarufi,
udondoshaji wa silabi katika neno, umoja na wingi na upachikaji wa silabi katika
neno. Halikadhalika, matokeo ya utafiti huu yameonesha mbinu ambazo walimu
wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza
katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni ni mbinu ya kurudiarudia, ishara,
kumshirikisha mwanafunzi, picha, mwalimu mwenyewe, chati na maandishi. Pia
matokeo yameonesha mitazamo chanya ya walimu kuhusu kupendelea kutumia mbinu
hizo kama vile kumrahisishia mjifunzaji lugha kutorejea makosa aliyofanya,
kumpunguzia hofu mwanafunzi na kumuongezea mwanafunzi msamiati mpya.
Mapendekezo yaliotolewa ni kuwa walimu wapewe mafunzo ya mara kwa mara
kuhusu mbinu mbalimbali zinazotumiwa katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika
stadi ya kuzungumza. Usahihishaji wa makosa uwe kwa makosa makubwa ambayo
yanazuia mazungumzo kwa kiasi kikubwa kwa kukosekana usahihi na ufasaha wa
lugha lengwa. Sambamba na hayo mtafiti ameshauri tafiti nyengine zifanyike katika
stadi ya kuandika na kusoma ili kuziba pengo lililoachwa na mtafiti hususani katika
usahihishaji wa makosa katika eneo la Kiswahili kama lugha ya kigeni
Description
Malengo ya utafiti huu ni kubainisha makosa ya kisarufi ambayo walimu wanayasahihisha zaidikatika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni, kueleza mbinu ambazo walimu wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni na kufafanua mitazamo ya walimu juu ya mbinu wanazozipendelea kutumia katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni