USAHIHISHAJI WA MAKOSA YA KISARUFI KATIKA STADI YA KUZUNGUMZA KATIKA DARASA LA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI

No Thumbnail Available
Date
2020-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu usahihishaji wa makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti huu umefanyika katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) katika kampasi ya Vuga, Zanzibar. Malengo ya utafiti huu ni kubainisha makosa ya kisarufi ambayo walimu wanayasahihisha zaidi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni, kueleza mbinu ambazo walimu wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni na kufafanua mitazamo ya walimu juu ya mbinu wanazozipendelea kutumia katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni. Nadharia ya Uchanganuzi Makosa iliyoasisiwa na Corder (1967) imetumika kuongozea utafiti huu. Data za msingi zimepatikana kwa njia ya ushuhudiaji, mahojiano na majadiliano. Watoa taarifa walikuwa ni walimu wanane wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha awali na kiwango cha kati. Matokeo yameonesha makosa ya kisarufi ambayo walimu wameyasahihisha zaidi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni ni makosa ya mpangilio wa vipashio usiostahiki, njeo, upatanisho wa kisarufi, udondoshaji wa silabi katika neno, umoja na wingi na upachikaji wa silabi katika neno. Halikadhalika, matokeo ya utafiti huu yameonesha mbinu ambazo walimu wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni ni mbinu ya kurudiarudia, ishara, kumshirikisha mwanafunzi, picha, mwalimu mwenyewe, chati na maandishi. Pia matokeo yameonesha mitazamo chanya ya walimu kuhusu kupendelea kutumia mbinu hizo kama vile kumrahisishia mjifunzaji lugha kutorejea makosa aliyofanya, kumpunguzia hofu mwanafunzi na kumuongezea mwanafunzi msamiati mpya. Mapendekezo yaliotolewa ni kuwa walimu wapewe mafunzo ya mara kwa mara kuhusu mbinu mbalimbali zinazotumiwa katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza. Usahihishaji wa makosa uwe kwa makosa makubwa ambayo yanazuia mazungumzo kwa kiasi kikubwa kwa kukosekana usahihi na ufasaha wa lugha lengwa. Sambamba na hayo mtafiti ameshauri tafiti nyengine zifanyike katika stadi ya kuandika na kusoma ili kuziba pengo lililoachwa na mtafiti hususani katika usahihishaji wa makosa katika eneo la Kiswahili kama lugha ya kigeni
Description
Malengo ya utafiti huu ni kubainisha makosa ya kisarufi ambayo walimu wanayasahihisha zaidikatika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni, kueleza mbinu ambazo walimu wanazitumia zaidi katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni na kufafanua mitazamo ya walimu juu ya mbinu wanazozipendelea kutumia katika kusahihisha makosa ya kisarufi katika stadi ya kuzungumza katika darasa la Kiswahili kama lugha ya kigeni
Keywords
Citation