Taathira za Ubabedume kwa Mwanamme Mwenza wa Kizanzibari Kupitia Nyimbo za Taarab Asilia

No Thumbnail Available
Date
2018-12
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
The State University of Zanzibar (SUZA)
Abstract
Tasnifu hii imelenga kuchunguza taathira za ubabedume kwa mwanamme mwenza wa Kizanzibari kupitia nyimbo za taarab asilia. Data zilikusanywa, zilichanganuliwa na matokeo yakabainishwa. Sura ya kwanza imebainisha usuli wa mada na tatizo la utafiti, ambalo ni uwelewa mdogo wa jamii kuhusu taathira za ubabedume kwa mwanamme mwenza katika jamii ya Wazanzibari. Utafiti uliongozwa na lengo kuu na malengo mahsusi. Sura ya pili ilizungumzia kazi tangulizi, mapitio kuhusiana na ubabedume, nyimbo na mapitio ya nyimbo za taarab. Aidha, ilizungumzia Nadharia ya mwitiko wa Msomaji na Nadharia ya Semiotiki. Sura ya tatu, ilionesha mbinu ya mahojiano iliyotumika kukusanyia data na hatua za mchanganuo wake. Mbinu ya maelezo ilitumika katika kuchanganua data na kupewa vifupisho. Sura ya nne imebainisha ubabedume ulivyojitokeza, uchambuzi wa taathira zake na hatua za kupambana na taathira hizo. Sura ya tano imeeleza kwa ufupi matokeo ya utafiti ambayo yamejitokeza kwa namna mbili, nyimbo zenye ubabedume wa wazi na zenye ubabedume uliojificha. Ndani yake mmejitokeza ubabedume wa kejeli, masikitiko, kuumiza moyo, malumbano na kutahadharisha. Pia taathira za woga, visasi, maradhi, msongo wa mawazo na kuhalalisha maovu. Utafiti umependekeza hatua za kuchukuwa kupunguza kasi ya ubabedume kwa mwanamme mwenza, kupewa taaluma kwa kutumia vyombo vya habari, kuwekea vitengo vya kushughulikiwa matatizo yao. Kazi hii imechangia kuongeza taaluma ya ubabedume kwa mwanamme katika jamii ya Wazanzibari. Hitimisho na mapendekezo ya utafiti uliofanyika yameoneshwa kwa ajili ya tafiti zijazo.
Description
Available in print form, Tunguu Reference Library
Keywords
1. Ubabedume - Nyimbo za Taarab Asili 2. Mwanamme wa Kizanzibar na nyimbo taarab asilia
Citation