UWIANO KATI YA MALENGO MAHSUSI NA MAZOEZI YA STADI YA KUZUNGUMZA KATIKA DARASA LA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI:
No Thumbnail Available
Date
2022-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu Uwiano kati ya Malengo Mahsusi na Mazoezi ya Stadi ya Kuzungumza katika Darasa la Kiswahili kama lugha ya Kigeni: Kitabu cha Zungumza Kiswahili: Hatua ya Kwanza (SUZA). Utafiti ulikuwa na malengo matatu ambayo ni; kwanza, kubainisha malengo mahsusi yaliyomo kwenye kitabu cha Zungumza Kiswahili: Hatua ya Kwanza. Pili, kuainisha mazoezi ya stadi ya kuzungumza yaliyotolewa na walimu wakati wa kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni. Tatu, kuonesha uwiano baina ya malengo mahsusi yaliyomo kwenye kitabu na mazoezi ya stadi ya kuzungumza yaliyotolewa darasani kwa wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti ulifanyika katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Utafiti uliongozwa na nadharia mbili ambazo ni; nadharia ya Mgao wa Viwango vya Ujifunzaji iliyoasisiwa na Benjamin Bloom na nadharia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na S. F. Scudder. Utafiti ulitumia mbinu ya ushuhudiaji na uchambuzi wa nyaraka katika kupata data zenye uhakika za utafiti huu. Aidha, mtafiti alitumia mkabala mseto. Sampuli ya watoa taarifa walikuwa ni walimu 6 naofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha kwanza. Matokeo yanaonesha kuwa kwa kiasi kikubwa walimu wanaongozwa na malengo mahsusi yaliyomo kwenye kitabu katika ufundishaji wao. Vilevile, uchunguzi umegundua kuwa, kwa kiasi kikubwa (61%) mazoezi ya stadi ya kuzungumza yaliyotolewa na walimu darasani yaliwiana na malengo mahsusi yaliyomo kwenye kitabu. Mapendekezo yaliyotolewa ni pamoja na Idara ya Kiswahili kwa Wageni kufanya marekebisho ya kitabu cha kufundishia kwa kuongeza baadhi ya malengo mahsusi katika mada ambazo zina lengo mahsusi moja au mawili kama vile mada ya Maamkizi, walimu kuhakikisha hawaachi kufuata malengo mahsusi ya kwenye kitabu kwani ndio yanayotoa muongozo
wa jinsi ya kufundisha mada zilizopangwa na mwisho mtafiti ameshauri kufanyika kwa tafiti nyengine ili kuziba pengo lilioachwa la uwiano katika stadi nyengine ambazo ni stadi ya kusoma, kuandika na kusikiliza.
Description
Utafiti uliongozwa na nadharia mbili ambazo ni; nadharia ya Mgao wa Viwango vya Ujifunzaji iliyoasisiwa na Benjamin Bloom na nadharia ya Mawasiliano iliyoasisiwa na S. F. Scudder. Utafiti ulitumia mbinu ya ushuhudiaji na uchambuzi wa nyaraka katika kupata data zenye uhakika za utafiti huu. Aidha, mtafiti alitumia mkabala mseto. Sampuli ya watoa taarifa walikuwa ni walimu 6
wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha kwanza. Matokeo yanaonesha kuwa kwa kiasi kikubwa walimu wanaongozwa na malengo mahsusi yaliyomo kwenye kitabu katika ufundishaji wao