Tathmini ya Mazingira ya Kijamii katika Kujifunza Kusoma Kiswahili kwa Watoto wa Kigeni Zanzibar

No Thumbnail Available
Date
2019-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu umetathmini Mazingira ya Kijamii katika kujifunza kusoma kwa watoto wa kigeni wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni Zanzibar. Jumla ya watoa taarifa 28 walishiriki katika utafiti huu waliogawanyika katika makundi mawili: wajifunzaji lugha 16 na wazazi/walezi wao 12. Utafiti ulifanyika katika skuli ya Kimataifa ya Feza iliyopo Mjini Magharib Zanzibar na katika kaya za wazazi/walezi wa wajifunzaji lugha ya Kiswahili zilizopo Mjini Magharib. Katika kukusanya data, utafiti umetumia kipimo cha kusoma ili kubaini uwezo walionao watoto wa kigeni katika kusoma matini za Kiswahili pamoja na mbinu ya usaili kubaini dhima ya Mazingira ya Kijamii. Aidha, utafiti ulitumia hojaji za kuchunguza mambo ya Mazingira ya Kijamii wa watoto wa kigeni. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Ukuzaji Stadi ya Kusoma ya Clay (1966) na Holdaway (1979). Hoja kuu ya nadharia hii ni mchangamano wa kimazungumzo na kusoma pamoja baina ya anayejifunza kusoma na wajuzi wa lugha husika. Vilevile, mchangamano baina ya mjifunzaji kusoma na vitabu vya lugha lengwa ni miongoni mwa misingi mikuu ya ujifunzaji kusoma kwa mujibu wa Nadharia ya Ukuzaji Stadi ya Kusoma. Matokeo ya utafiti yanaonesha kwamba dhima ya Mazingira ya Kijamii katika kujifunza kusoma Kiswahili kwa watoto wa kigeni ni kuwawezesha watoto kupata kuchanganyika na marafiki wanaojua Kiswahili wakiwa katika Mazingira ya Kijamii. Aidha, kuchanganyika na wazazi/walezi wanaotumia Kiswahili pamoja na tabia binafsi ya watoto kujisomea maandiko ya Kiswahili wakiwa katika Mazingira ya Kijamii pia vimechangia uwezo wa kusoma walionao watoto wa kigeni. Vilevile, imependekezwa kwa watafiti wengine kufanyika utafiti kuhusu ufundishaji na ujifunzaji wa stadi nyengine za lugha ya Kiswahili katika Mazingira ya nje na ndani ya darasa.
Description
TATHMINI YA MAZINGIRA YA KIJAMII KATIKA KUJIFUNZA KUSOMA KISWAHILI KWA WATOTO WA KIGENI ZANZIBAR
Keywords
TATHMINI YA MAZINGIRA YA KIJAMII KATIKA KUJIFUNZA KUSOMA KISWAHILI KWA WATOTO WA KIGENI ZANZIBAR
Citation