TATHMINI YA MSINGI WA UHALISIA KATIKA MITIHANI YA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI:

No Thumbnail Available
Date
2021-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu wenye mada Tathmini ya Msingi wa Uhalisia katika Mitihani yaKiswahili kama Lugha ya Kigeni: Mfano Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Lengo kuu la utafiti huu ni kutathmini kwa kiasi gani msingi wa uhalisia unavyofikiwa katika mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni. Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa mawili. Moja, ni kubainisha uelewa kwa walimu kuhusu msingi wa uhalisia katika kuandaa mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni. Lengo la pili lilikuwa ni kufafanua kiwango cha msingi wa uhalisia kinavyofikiwa katika mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Umahiri wa Kimawasiliano iliyoasisiwa na Hymes (1972) na kuendelezwa na Canale na Swain (1980 - 1983). Katika kukusanya data, utafiti huu ulitumia mbinu ya hojaji na uchambuzi wa nyaraka. Vilevile, utafiti ulitumia modeli ya Bachman na Palmer (1996) iliyobainisha tabia oanishi kati ya Lugha Lengwa Tumizi (LLT) na Lugha Tumizi ya Mtihani (LTM). Jumla ya nyaraka nne kutoka Idara ya Kiswahili kwa Wageni (SUZA) zilitumika kupata data za utafiti huu. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha kiasi wastani cha uelewa wa walimu kuhusu msingi wa uhalisia katika uandaaji mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni. Sambamba na hilo, utafiti ulionesha na kufafanua kwamba msingi wa uhalisia haukuzingatiwa vyema. Imependekezwa kuwa msingi wa uhalisia katika uandaaji mitihani ya Kiswahili kwa wageni ni muhimu kuzingatiwa ipasavyo. Pia, walimu wanaofundisha lugha hiyo ni vizuri kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu msingi wa uhalisia na kuutumia katika uandaaji mitihani inayowapima wanafunzi aina hiyo. Hivyo, ni vyema kufanyika utafiti kwa misingi mengine ili mitihani ya iswahili kama lugha ya kigeni iweze kukidhi viwango vinavyohitajika sasa katika upimaji wa lugha za kigen
Description
Malengo mahsusi ya utafiti huu yalikuwa mawili. Moja, ni kubainisha uelewa kwa walimu kuhusu msingi wa uhalisia katika kuandaa mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni. Lengo la pili lilikuwa ni kufafanua kiwango cha msingi wa uhalisia kinavyofikiwa katika mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni
Keywords
Citation