Mikakati binafsi ya Kujifunza Lugha Inayomsaidia Mwanafunzi wa Kigenu Kuzungumza Lugha ya Kiswahili
No Thumbnail Available
Date
2019-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
IKISIRI
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mikakati binafsi ya kujifunza lugha inayomsaidia mwanafunzi wa kigeni kuzungumza lugha ya Kiswahili. Utafiti ulifanyika Zanzibar katika kisiwa cha Unguja katika Mkoa wa Kusini Unguja na Mkoa wa Mjini Magharibi. Utafiti huu una malengo mahususi matatu ambayo ni kuelezea mitazamo ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni wakati wanapojiwekea mikakati yao binafsi ya kujifunza kuzungumza lugha ya Kiswahili. Kutathmini ni kwa kiasi gani wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni wanatumia mikakati binafsi katika kujifunza kuzungumza Kiswahili. Kubainisha mikakati binafsi ambayo ni sahihi inayotumiwa na wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni ambayo inawawezesha kuweza kuzungumza lugha ya Kiswahili. Jumla ya walengwa wa utafiti huu ni watafitiwa (15) ambao ni wastani wa (75%). Watafitiwa hawa walipatikanwa katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar, Taasisi ya Mafunzo ya Kiswahili ya Paje na wageni ambao tayari wameshajifunza Kiswahili wamepatikana maeneo ya Mji Mkongwe kwa kutumia uteuzi wa usampulishaji rahisishi. Hojaji na Usaili zilitumika kama mbinu za kukusanyia data za utafiti huu. Mtafiti alitumia nadharia ya Utamaduni Jamii na nadharia Tete Ingizo. Data zilipatikanwa uwandani na zilifafanuliwa kwa kutumia mkabala wa mseto. Matokeo ya utafiti huu yalionesha kuwa (93.3%) ya wanafunzi wanaojifunza kuzungumza lugha ya Kiswahili wanatumia mikakati binafsi na mikakati hiyo ni sahihi lakini hawana uelewa wa kutosha wa utumiaji wa mikakati ya kujifunza lugha. Asilimia kubwa ya watafitiwa hutumia mkakati jamii katika kujifunza kwao. Mtafiti amependekeza kwa watafiti wengine kuchunguza mikakati binafsi ya kujifunza lugha ambayo humsaidia mwanafunzi wa kigeni kusikiliza, kusoma na kuandika. Pia watafiti wachunguze mikakati binafsi wanayoitumia walimu katika kuwafundisha wanafunzi wa kigeni lugha ya Kiswahili. Pendekezo jingine ni kwa Uongozi wa chuo ama taasisi waweke program endelevu ya rafiki lugha ili mwanafunzi aweze kuzungumza kwa haraka zaidi na kuujuwa utamaduni wa lugha ya Kiswahili.
Description
Utafiti huu ulilenga kuchunguza mikakati binafsi ya kujifunza lugha inayomsaidia mwanafunzi wa kigeni kuzungumza lugha ya Kiswahili. Utafiti ulifanyika Zanzibar katika kisiwa cha Unguja katika Mkoa wa Kusini Unguja na Mkoa wa Mjini Magharibi. Utafiti huu una malengo mahususi matatu ambayo ni kuelezea mitazamo ya wanafunzi wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni wakati wanapojiwekea mikakati yao binafsi ya kujifunza kuzungumza lugha ya Kiswahili
Keywords
MIKAKATI BINAFSI YA KUJIFUNZA LUGHA INAYOMSAIDIA MWANAFUNZI WA KIGENI KUZUNGUMZA LUGHA YA KISWAHILI