TATHMINI YA UTHABITI WA MITIHANI YA KISWAHILI KWA WAGENI:

No Thumbnail Available
Date
2020-12-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulihusu Tathmini ya Uthabiti wa Mitihani ya Kiswahili Kwa WageniMfano Mitihani Kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Utafiti huu ulilenga kuchunguza iwapo mitihani nayotayarishwa kwa ajili ya wanafunzi wageni ni thabiti kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na malengo mahsusi mawili ambayo ni: Kupambanua iwapo mitihani imeakisi maudhui ya kujifunza Kiswahili kwa wageni katika kiwango cha awali na kutathmini iwapo mitihani ya Kiswahili kwa wageni katika kiwango cha awali imepima stadi za lugha kama inavyotakiwa. Utafiti huu ulifanyika katika Idara ya Kiswahili kwa wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Kanuni ya uthabiti na nadharia ya upimaji wa lugha kimawasiliano ziliongoza utafiti huu. Utafiti ulihusisha mbinu ya uchambuzi wa nyaraka na usaili katika ukusanyaji wa data. Mitihani ya miaka minne tofauti, muhutasari, kitabu cha Zungumza Kiswahili Hatua ya Kwanza na walimu watano kutoka Idara ya Kiswahili kwa wageni walitumika kama sampuli ya utafiti. Data za utafiti ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti yalikuwa kama ifuatavyo: Kwa upande wa lengo la kwanza, matokeo yanaonesha kwamba mitihani imeakisi maudhui ya kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha awali. Hii ni kwa sababu masuala yote yaliyojitokeza katika mitihani kama vile mada, mitindo ya matini, urefu wa matini, sarufi na mazoezi yaliyojitokeza katika mitihani ni sehemu ya masuala yaliyopendekezwa kwa mwanafunzi wa Kiswahili kama lugha ya kigeni wa kiwango cha awali. Kwa upande wa lengo la pili, mitihani ilifanikiwa kupima ujuzi wa kusoma na kuandika kwani mazoezi ya kusoma kwa ufahamu na uandishi yaliyomo katika mitihani yamepima dhahiri pia yameakisi uhalisia wa ujuzi wa kusoma na kuandika. Aidha, utafiti umebaini mitihani ilijumuisha mazoezi ya kupima usahihi wa kanuni za lugha badala ya upimaji wa vipengele hivyo kuakisi uhalisia wa namna vinavyotumika kama nadharia ya upimaji wa lugha mawasiliano inavyoelekeza. Kutokana na matokeo hayo, utafiti ulipendekeza kuimarishwa kwa utungaji wa mitihani ya lugha pamoja na kufanyika utafiti fuatishi kuhusu kanuni nyengine za upimaji wa lugha kwa mitihani ya Kiswahili kama lugha ya kigeni ili kubaini kwa namna gani mitihani hiyo inazingatia kanuni za upimaji bora wa lugha kama inavyopendekezwa
Description
Utafiti huu ulifanyika katika Idara ya Kiswahili kwa wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Kanuni ya uthabiti na nadharia ya upimaji wa lugha kimawasiliano ziliongoza utafiti huu. Utafiti ulihusisha mbinu ya uchambuzi wa nyaraka na usaili katika ukusanyaji wa data. Mitihani ya miaka minne tofauti, muhutasari, kitabu cha Zungumza Kiswahili Hatua ya Kwanza na walimu watano kutoka Idara ya Kiswahili kwa wageni walitumika kama sampuli ya utafiti. Data za utafiti ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo.
Keywords
Citation