Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari zake kwa Watoto Zanzibar

dc.contributor.authorHAFIDH, Zainab Ali
dc.date.accessioned2020-08-19T08:36:01Z
dc.date.available2020-08-19T08:36:01Z
dc.date.issued2018-01
dc.descriptionAvailable in print form, Tunguu Reference Libraryen_US
dc.description.abstractUtafiti huu unazungumzia “Matumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari Zake kwa Watoto Zanzibar”. Matumizi ya lugha katika jamii yameonekana kuwa yanatumika kwa namna tafauti. Hali hii imedhihirika kutokana na makundi mbalimbali yaliomo ndani ya jamii. Tafauti za kijinsi, elimu, rika, uhusiano wa wazungumzaji na muktadha, ndio sababu ya kuwepo kwa makundi katika jamii, yanayoleta tafauti hiyo katika lugha. Wazee wa kike kama kundi lilioko katika jamii, watakuwa na namna yao ya kutumia lugha wanapowasiliana na watoto wao. Ili kujua sifa, muktadha wa matumizi na athari za lugha hiyo kwa watoto wao Zanzibar, utafiti huu una lengo la kuchunguza matumizi ya lugha ya wazee wa kike na athari zake kwa watoto.Utafiti umeongozwa na nadharia ya kijamii ya Fishman (1972) ambapo msingi wake mkuu ni lugha na matumizi yake katika jamii. Data za utafiti huu zilikusanywa kutumia mbinu ya mahojiano, uchunguzi makinifu na uchunguzi shirikishi. Matokeo yameonesha kuwa lugha ya wazee wa kike ina sifa mbalimbali, sifa ambazo zimegawika katika kiwango cha msamiati, sentensi na maana. Aidha wazee wa kike hutumia lugha kwa mujibu wa muktadha wa jambo husika na pia imebainika kuwa lugha ya wazee wa kike ina athari chanya na hasi kwa watoto. Kutokana na matokeo hayo inapendekezwa kuwa wazee wa kike wa kizanzibari watumie lugha kwa mujibu wa mila na desturi za jamii husika. Na pia kuanzishwe chombo maalumu kitakachoshughulikia matumizi ya lugha katika vyombo vya kukuza lugha ya Kiswahilien_US
dc.identifier.urihttp://repository.suza.ac.tz:8080/xmlui/handle/123456789/158
dc.language.isootheren_US
dc.publisherThe State University of Zanzibar (SUZA)en_US
dc.subject1. Matumizi ya Lugha - Wazee wa kike 2. Athari ya matumizi ya Lugha kwa watoto - Zanzibaren_US
dc.titleMatumizi ya Lugha ya Wazee wa Kike na Athari zake kwa Watoto Zanzibaren_US
dc.typeThesisen_US
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
UTAFITI MAREKEBISHo ya mwisho FINAL.pdf
Size:
786.25 KB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: