CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI KATIKA STADI YA KUSOMA

dc.contributor.authorKHALFAN, Shani Suleiman
dc.date.accessioned2024-04-18T08:26:51Z
dc.date.available2024-04-18T08:26:51Z
dc.date.issued2019-12-12
dc.descriptionLengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza changamoto zinazowakabili walimu katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Stadi ya Kusoma
dc.description.abstractLengo kuu la utafiti huu ni kuchunguza changamoto zinazowakabili walimu katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Stadi ya Kusoma. Utafiti huu umefanywa katika Idara ya Kiswahili kwa Wageni ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Kituo cha Kiswahili na Utamaduni (KIU) katika tawi lake la Zanzibar. Mtafiti alitumia nadharia ya stadi ya kusoma ya Schema iliyoasisiwa na Barlett (1932) na kuungwa mkono na Rumelhart na Ortony (1977). Washiriki wa utafiti huu walikuwa ni walimu wanaofundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni katika Chuo Kikuu cha Zanzibar, Idara ya Kiswahili kwa Wageni na Kituo cha Kiswahili na Utamaduni. Mbinu za ukusanyaji data alizotumia mtafiti katika utafiti huu ni dodoso, usaili na ushuhudiaji. Matokeo ya utafiti yamebaini kuwa walimu wanakabiliwa na changamoto nyingi katika ufundishaji wa stadi ya kusoma; kama ukosefu wa vifaa vya kufundishia, walimu kukosa mbinu za kisasa katika ufundishaji na ugumu wa matini zinazotumika kufundishia stadi ya kusoma. Changamoto hizo zimesababisha walimu kuumia muda mwingi katika ufundishaji, kutofikia malengo ya ufundishaji waliyojiwekea, kukosa ari, hamu na shauku ya kuendelea kufundisha na kutumia nguvu za ziada. Utafiti huu umetoa apendekezo kuwa ili ufundishaji wa stadi ya kusoma uwe na ufanisi, taasisi husika zinapaswa kutoa mafunzo ya mara wa mara kwa walimu, uandaaaji wa vifaa vya kisasa vya ufundishaji vinavyokwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia ya ufundishaji lugha. Walimu wajijengee tabia ya kujisomea na kujifunza kupitia mitandao badala ya kusubiri nafasi za ufadhili.
dc.description.sponsorshipSUZA
dc.identifier.otherTHESIS
dc.identifier.urihttps://repository.suza.ac.tz/handle/123456789/246
dc.publisherSUZA
dc.relation.ispartofseries2019
dc.titleCHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI KATIKA STADI YA KUSOMA
dc.typeThesis
Files
Original bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU KATIKA UFUNDISHAJI WA KISWAHILI KAMA LUGHA YA KIGENI KATIKA STADI YA KUSOMA.pdf
Size:
2.43 MB
Format:
Adobe Portable Document Format
Description:
License bundle
Now showing 1 - 1 of 1
Loading...
Thumbnail Image
Name:
license.txt
Size:
1.71 KB
Format:
Item-specific license agreed upon to submission
Description: