USAWIRI WA MWANAMKE KATIKA NYIMBO ZA KIDUMBAKI ZANZIBAR.

No Thumbnail Available
Date
2020-03-01
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu unahusu Usawiri wa Mwanamke katika Nyimbo za Kidumbaki Zanzibar. Data zilikusanywa zilichanganuliwa na matokeo yamebainishwa. Sura ya kwanza ilikuwa ni usuli wa mada, tatizo la utafiti, malengo mahususi pamoja na umuhimu wa utafiti huo. Sura ya pili ilizungumzia kazi tangulizi kuhusiana na taswira ya mwanamke. Aidha sura hii imezungumzia nadharia ya Ufeministi na Mwitiko wa Msomaji. Sura ya tatu mtafiti alitumia mbinu ya usaili, dodoso na ushuhudiaji. Mbinu ya maelezo imetumika katika kuchambua data. Sura ya nne imebainisha baadhi ya nyimbo za kidumbaki ambazo zimemsawiri mwanamke, imeonesha usawiri hasi na chanya, pamoja na sababu zilizo wafanya watunzi kumsawiri mwanamke. Sura ya tano imeeleza kwa ufupi matokeo ya utafiti, mchango mpya wa utafiti, changamoto za utafiti na utatuzi wake, pamoja na mapendekezo ya jumla. Kwa hivyo, utafiti huu umeweza kubainisha sababu na chanzo cha usawiri hasi na chanya wa mwanamke katika nyimbo za kidumbaki. Nyimbo mbalimbali za kidumbaki ndizo chanzo cha data za utafiti na ambazo zimechunguzwa na kuchambuliwa. Utafiti umefanyika katika Mkoa wa Mjini Magharibi. Malengo ya utafiti huu ni matatu. La kwanza, kubainisha mashairi ya nyimbo za kidumbaki yenye kumsawiri mwanamke, la pili ni kuchunguza usawiri hasi na chanya wa mwanamke katika nyimbo za kidumbaki.Lengo la mwisho ni kubainisha sababu zinazowafanya watunzi wa nyimbo za kidumbaki kumsawiri mwanamke katika nyimbo zao. Mtafiti ametumia nadharia ya Ufeministi na Mwitiko wa Msomaji katika ukusanyaji na uchambuzi wa data. Nadharia zimesibu katika kutanzua tatizo la utafiti. Uchambuzi wa data umeonesha matokeo ya kuwa mwanamke katika nyimbo hizi anasawiriwa katika mitazamo miwili ya hasi na chanya. Vile vile sababu zimebainishwa katika utafiti huu
Description
Utafiti huu unahusu Usawiri wa Mwanamke katika Nyimbo za Kidumbaki Zanzibar.
Keywords
Citation