TATHMINI YA UTHABITI WA MITIHANI YA KISWAHILI KWA WAGENI:
Loading...
Date
2020-12-01
Authors
Journal Title
Journal ISSN
Volume Title
Publisher
SUZA
Abstract
Utafiti huu ulihusu Tathmini ya Uthabiti wa Mitihani ya Kiswahili Kwa Wageni:
Mfano Mitihani Kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Utafiti huu ulilenga
kuchunguza iwapo mitihani inayotayarishwa kwa ajili ya wanafunzi wageni ni
thabiti kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa. Utafiti huu uliongozwa na
malengo mahsusi mawili ambayo ni: Kupambanua iwapo mitihani imeakisi maudhui
ya kujifunza Kiswahili kwa wageni katika kiwango cha awali na kutathmini iwapo
mitihani ya Kiswahili kwa wageni katika kiwango cha awali imepima stadi za lugha
kama inavyotakiwa. Utafiti huu ulifanyika katika Idara ya Kiswahili kwa wageni ya
Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar. Kanuni ya uthabiti na nadharia ya upimaji wa
lugha kimawasiliano ziliongoza utafiti huu. Utafiti ulihusisha mbinu ya uchambuzi
wa nyaraka na usaili katika ukusanyaji wa data. Mitihani ya miaka minne tofauti,
muhutasari, kitabu cha Zungumza Kiswahili Hatua ya Kwanza na walimu watano
kutoka Idara ya Kiswahili kwa wageni walitumika kama sampuli ya utafiti. Data za
utafiti ziliwasilishwa kwa njia ya maelezo. Matokeo ya utafiti yalikuwa kama
ifuatavyo: Kwa upande wa lengo la kwanza, matokeo yanaonesha kwamba mitihani
imeakisi maudhui ya kujifunza Kiswahili kama lugha ya kigeni katika kiwango cha
awali. Hii ni kwa sababu masuala yote yaliyojitokeza katika mitihani kama vile
mada, mitindo ya matini, urefu wa matini, sarufi na mazoezi yaliyojitokeza katika
mitihani ni sehemu ya masuala yaliyopendekezwa kwa mwanafunzi wa Kiswahili
kama lugha ya kigeni wa kiwango cha awali. Kwa upande wa lengo la pili, mitihani
ilifanikiwa kupima ujuzi wa kusoma na kuandika kwani mazoezi ya kusoma kwa
ufahamu na uandishi yaliyomo katika mitihani yamepima dhahiri pia yameakisi
uhalisia wa ujuzi wa kusoma na kuandika. Aidha, utafiti umebaini mitihani
ilijumuisha mazoezi ya kupima usahihi wa kanuni za lugha badala ya upimaji wa
vipengele hivyo kuakisi uhalisia wa namna vinavyotumika kama nadharia ya
upimaji wa lugha mawasiliano inavyoelekeza. Kutokana na matokeo hayo, utafiti
ulipendekeza kuimarishwa kwa utungaji wa mitihani ya lugha pamoja na kufanyika
utafiti fuatishi kuhusu kanuni nyengine za upimaji wa lugha kwa mitihani ya
Kiswahili kama lugha ya kigeni ili kubaini kwa namna gani mitihani hiyo
inazingatia kanuni za upimaji bora wa lugha kama inavyopendekezwa
Description
Utafiti huu ulilenga kuchunguza iwapo mitihani inayotayarishwa kwa ajili ya wanafunzi wageni ni thabiti kulingana na madhumuni yaliyokusudiwa.